Je, inahisije kuwa Bingwa wa Chakula wa Umoja wa Mataifa?
Nimekutana na watu ambao wamebadilisha mawazo yangu na kunitia moyo kuendelea na ukuaji na kuzidi kuleta maendeleo kama mmoja wa mabingwa wa chakula ulimwenguni kote. Kufikia sasa, tumeanzisha karibu Mikutano 41 Huru ya wa Mfumo wa Chakula katika nchi wanachama wa Muungano wa Vijana wa Kilimo Bora kwa Hali ya Hewa (CSAYN) barani Afrika.
Je, matarajio yako ni nini?
Matarajio yangu binafsi mwanzoni yalikuwa kukutana na kushirikiana na vijana kote barani Afrika na ulimwenguni. Vivyo hivyo, nilitaka kuwa bingwa bora na mwenye ushawishi mkubwa wa chakula kwa kuandaa Mikutano mingine iwezekanavyo kujadili mifumo ya chakula.
Je, umetimiza nini kufikia sasa?
Niliweza kuanzisha hifadhidata ya Mashujaa wa Mifumo ya Chakula (FSSH), ambayo sasa ina washiriki 792 ulimwenguni. Tulianzisha zaidi ya Mikutano Huru 41 ya Mifumo ya Chakula kote ulimwenguni na bado tunaendelea; na tulianzisha makao ya kusasisha na kuratibu juhudi na Umoja wa Mataifa kuhusu Mkutano huu. Tuliandaa pia Mikutano miwili ya ngazi ya juu ya Mifumo ya Chakula, ambayo ilivutia watu wapatao 700.
Kuridhika kwangu zaidi kibinafsi ni kuwa CSAYN Global imepata mvuto ulimwenguni kote, na kuwa muungano wa kurejelewa. Kwa hivyo, vijana wengi wanafurahia kujiunga na muungano huu kwa sababu ya ukuaji mkubwa kutoka nchi nne mwaka wa 2014 hadi nchi 90 kufikia Mei 2021.