Ekari 150 za mashamba ya migomba zateketea kwa moto Torit Sudan Kusini
Get monthly
e-newsletter
Ekari 150 za mashamba ya migomba zateketea kwa moto Torit Sudan Kusini
Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini , UNMISS umesema ekari 150 za mashamba ya migomba zimeteketea kwa moto wa nyika kwenye eneo la Iyere Payam katika jimbo la Torit nchini humo.
Moto huo ulibainiwa na walinda amani wa UNMISS waliokuwa wakishika doroa katika maeneo ya Haramorok na Hafayi Bomas jimboni Torit Magharibi mwa Sudan Kusini.
Kwa mujibu wa UNMISS mashamba hayo yaliyoteketea wiki hii yalitelekezwa mwaka 2017 wakati wakulima walipofungasha virago kukimbia mapigano baina ya vikosi vyenye silaha na hadi sasa ni wakazi wachache tu walioweza kurejea katika maeneo hayo.
Akizungumzia athari za moto huyo wa nyika kwa jamii husika chifu wa Haramorok boma bwana Lino Owor Augustino amesema tukio hilo limeziacha familia za wakazi wanaorejea bila msaada wowote wa chakula wala malazi.
听