Umoja wa Afrika ulipopitisha Itifaki ya Haki za Wanawake barani Afrika (Itifaki ya Maputo) mwaka 2003, lengo lilikuwa kuimarisha haki za kibinadamu, kijamii, kiuchumi na kisiasa za wanawake katika bara hili ili waweze kuutimiza uwezo wao kamili.
Kupitia itifaki hiyo, wanawake wanatambulika kama wachangiaji muhimu katika mageuzi ya kijamii na kiuchumi na ustawi wa jamii zao. Mataifa Wanachama ya AU yana wajibu wa kubuni sera, mikakati na taratibu za kitaasisi ambazo zinaunda fursa sawa kwa wanawake, ikiwa ni pamoja na ndani ya sekta ya ardhi.
Mwaka 2009, Wakuu wa Mataifa na Serikali za Umoja wa Afrika walipitisha Azimio la Bunge (Assembly/AU/Decl.1(XIII) Rev.1) kuhusu Masuala ya Ardhi na Changamoto barani Afrika katika Mkutano wa 13 wa Kawaida huko Sirte, Libya, na kuanzisha Mkutano kuhusu Sera ya Ardhi Barani Afrika (CLPA) kama mjadala mkuu wa kisera na hafla ya kubadilishana taarifa kuhusu utekelezaji wa Ajenda ya AU kuhusu Ardhi Barani Afrika na kubainisha masuluhisho ya changamoto hizi.
Mnamo 2015, Kamati Maalumu ya Kiufundi ya AU ya Kilimo, Maendeleo Mashambani, Maji na Mazingira (STC-ARDWE) ilipitisha pendekezo lililolenga kusaidia uwezeshaji wa wanawake kiuchumi. Mataifa Wanachama yalitakiwa kubuni sera, sheria na taratibu nyingine ambazo zingeweza kuelekea kwenye ugawaji wa 30% ya ardhi iliyosajiliwa kwa wanawake.
Kamati ya nne ya kiufundi (STC-ARDWE) aidha ilipitisha Mkakati wa Utawala wa Ardhi wa AU kama Mkakati wa Bara wa kuiongoza Tume ya AU, Kituo cha Sera ya Ardhi cha Afrika, Jumuiya za Kiuchumi za Kikanda, Mataifa Wanachama na wahusika wasio wa kiserikali ili kufikia matarajio yaliyotajwa katika azimio hilo kuhusu Masuala ya Ardhi na Changamoto barani Afrika.
Utekelezaji
Utekelezaji wa Mkakati wa Utawala wa Ardhi wa AU unawajibikia hitaji la dharura la kushughulikia ufikiaji mdogo wa wanawake wa fedha zinazotegemeka na zinazotabirika na miundo ya masoko ambayo ni muhimu kwa uzalishaji bora katika kilimo na mifumo salama ya chakula, jukumu muhimu la wanawake katika shughuli za biashara za kikanda, ama kupitia biashara rasmi au kupitia shughuli zisizo rasmi na ndogondogo.
Mwongo wa Wanawake wa Umoja wa Afrika (2010 hadi 2020) ulionyesha mafanikio muhimu katika kilimo, ikiwa ni pamoja na kupanua ufikiaji wa wanawake kwa masoko; maji; ardhi, kupitia mfumo wa vyeti vya ardhi; ruzuku na pembejeo za kilimo.
AU ilizindua sanamu inayoashiria kujitolea kwa kampeni ya "Kurejesha Jembe kwenye Makavazi" katika mji wa Burkina-Faso wa Bobo-Dioulasso ambayoÌýiliashiria ajenda ya bara hili ya kukuza kilimo cha mashine miongoni mwa wanawake ili kuboresha uzalishaji wa chakula, biashara ya bidhaa za kilimo na huduma na kukuza kasi ya ahadi muhimu ya Agenda 2063.
Tayari, kuna mwelekeo chanya uliosajiliwa nchini Tanzania, Malawi na Uganda katika kupunguza pengo la kijinsia katika wanawake kumiliki ardhi na ushiriki wao katika uzalishaji wa kilimo. Kwa mfano, nchini Tanzania 32% ya wanawake ni wamiliki wa ardhi ikilinganishwa na 42% ya wanaume.
Hata hivyo, nchini Naijeria ni 4% tu ya wanawake, ikilinganishwa na 23% ya wanaume wanaomiliki ardhi ya kilimo. Nchini Nijer, 63% ya wanaume na 35% ya wanawake wanamiliki ardhi ya kilimo.
Katika nchi kama vile Benin, Burkina Faso, Cape Verde, Côte d'Ivoire, Gambia, Ghana, Guinea, Guinea-Bissau, Laiberia na Togo, chini ya humusi ya wanawake walimiliki ardhi mwaka 2021.
Ingawa kuna maendeleo katika baadhi ya nchi kwa utambuzi wa wazi wa haki sawa za wanawake, kukuza umiliki wa pamoja na usajili wa ardhi, kutunga sheria za kimaendeleo za urithi, ulinzi wa haki za kumiliki mali kwa wajane, bado mengi hayajafanywa. Kuna kuendelea kwa uwezo hafifu wa kitaasisi na mapungufu ya maarifa yanayohitajika kwa afua za kukabili hali zinazozingatia jinsia ili kuimarisha haki za ardhi za wanawake na usalama wa umiliki.
Umuhimu wa utafiti
Eneo la haraka la kuzingatia katika kuimarisha haki za ardhi za wanawake na usalama wa umiliki ni utafiti.
Utafiti unathibitisha kuwa umiliki salama wa ardhi kwa wanawake huongeza uwekezaji wa kilimo na uwezo wa kuingia katika mikataba ya kilimo. Hasa, utafiti umeonyesha kuwa usalama wa umiliki wa ardhi wa wanawake ni muhimu kwa uwezeshaji wao katika ngazi ndogo kama wazalishaji wa kilimo katika kaya na katika ngazi ya jumla kwa ajili ya kufungua manufaa ya mageuzi ya kijamii na kiuchumi.
Baadhi ya tafiti ziliangazia upatikanaji wa ardhi kwa wanawake, sera za mageuzi ya sheria na mikakati ya kuhakikisha upatikanaji wa ardhi na kuongeza uwezo wa Mataifa Wanachama kuunda sera wezeshi, mazingira ya kisheria, mfumo wa usimamizi wa ardhi unaozingatia jinsia ambao unaambatana na mabadiliko ya mitazamo ya kijamii na mfumo dume na mila zinazobana haki za ardhi za wanawake.
Teknolojia bunifu ya kidijitali inaweza kuhudumia haki za ardhi za wanawake na ushiriki wao katika kilimo kwa njia bora zaidi.
STC-ARDWE ya tano iliidhinisha Mkakati wa Kilimo wa Kidijitali wa Umoja wa Afrika pamoja na Mpango wake wa Utekelezaji wa 2024-2027 ili kupitishwa na kutoa wito kwa RECS na Mataifa Wanachama kuanzisha mipango ya kikanda ya kidijitali, miongoni mwayo ni kuondolewa kwa vikwazo vinavyozuia upatikanaji wa elimu ya kifedha ya kidijitali kwa wanawake na vijana.
Nchini Rwanda, kwa mfano, mpango wa "Nunua kutoka kwa Wanawake" umewainua wanawake wanapojihusisha na kilimo cha kidijitali. Mpango huo unaongeza ufikiaji wa masoko kwa kuunda majukwaa yaliyowezeshwa kidijitali ambayo yanawaunganisha wanawake na taarifa za biashara ya kilimo, vyombo vya kifedha na masoko ya bidhaa zao.
Kuna fursa za kuwekeza katika huduma za nyanjanii za kilimo ili kupeleka ujuzi na maarifa kwa utaratibu miongoni mwa wakulima wadogowadogo, wengi wao wakiwa wanawake, kwa kutumia teknolojia za kuhifadhi mazao ya kilimo pamoja na kushirikisha akili unde ili kuboresha usindikaji wa jumla wa kilimo na uongezaji thamani katika shughuli za kilimo cha wanawake, pamoja na kujenga ushirikiano imara katika masoko ya ndani na nje ya nchi pamoja na biashara ya mipakani.
Mojawapo ya malengo makuu ya Eneo Huru la Biashara la Bara Afrika (AfCFTA) ni "kukuza na kufikia maendeleo endelevu na shirikishi ya kijamii na kiuchumi, usawa wa kijinsia na mageuzi ya kimuundo ya Mataifa Wanachama".
AfCFTA inatoa fursa kwa ukuaji wa kiuchumi jumuishi wa Mataifa Wanachama ili kukuza uanuwai wa chumi na kuharakisha biashara ili kufikia uwekezaji zaidi katika kutekeleza masharti ya sheria za bara na maamuzi ambayo yanahitaji kulinda na kukuza haki za ardhi za wanawake.
Dkt. Janet Edeme - mwanasayansi wa kilimoÌýnaÌýmwanabayolojiaÌýwa mimea - ni Mkurugenzi katika Idara ya Uchumi wa Mashambani na Kilimo katikaÌýTume ya Umoja wa AfrikaÌý(AUC/DREA). @EdemeDr kwenye X