Ãå±±½ûµØ

Muongo wa Kuchukua Hatua: Kutatua mapungufu ya maendeleo Afrika

Get monthly
e-newsletter

Muongo wa Kuchukua Hatua: Kutatua mapungufu ya maendeleo Afrika

Mabadiliko katika itikadi, kujiendeleza baada ya Uviko-19 na kutumia ajenda ya malengo ya maendeleo endelevu (SDG) kunaweza kusaidia
Afrika Upya: 
3 February 2022
Trucks loaded with goods waiting for weeks to cross the C?te d¡¯Ivoire-Ghana borders at Elubo/Noe.
Franck Kuwonu/AR
Trucks loaded with goods waiting for weeks to cross the C?te d¡¯Ivoire-Ghana borders at Elubo/Noe.

Kwa miongo miwili iliyopita, Afrika imeendelea kuwa mwenyeji wa baadhi ya nchi zinazokua kwa haraka kiuchumi duniani, licha ya athari hasi za tandavu ya Uviko-19.

Frederick Mugisha
Frederick Mugisha

Tangu mwaka 2000, katika nchi 20 zinazokua kwa kasi zaidi kiuchumi duniani, Afrika inajumuisha kati ya nchi 3 na 12 - takwimu ambayo inayostahili kusherehekewa.

Afrika, hata hivyo, haiwezi kuridhika na takwimu hii ya kuvutia kwa sababu ya changamoto kuu ambazo zinazidi kulikumba bara hilli.?

Tuanze na pato la taifa (GDP), ambalo huonyesha maendeleo ya nchi.? Pato la taifa ni kipimo sahihi kinachotuambia jinsi nchi inavyozalisha kwa kila mwananchi wake.

Katika miaka ya 1960s, kati ya nchi 20 zilizokuwa na mapato ya chini zaidi, 14 zilikuwa barani Afrika. Na katika miaka ya 2010, kati ya nchi 20 zilizokuwa na mapato ya chini zaidi ya pato la taifa, 19 zilikuwa barani Afrika. Takwimu zinaonyesha kwamba, ingawa Afrika ilikuwa na uchumi unaokua kwa kasi, maendeleo hayakuwa makubwa kiuhalisia.

Tafiti nyingine zinatuambia hadithi kama hiyo. Mwaka 1990, wakati Kipimo cha Maendeleo ya Binadamu (HDI) kilikadiriwa kwa mara ya kwanza, kati ya nchi 20 zilizokuwa na HDI ya chini zaidi, 16 zilikuwa Afrika. Mwaka 2019, kati ya nchi 20 zilizokuwa na HDI ya chini zaidi, 18 zilikuwa Afrika.

Ligi ya soka

Kama nchi zingeweza kuwa sehemu ya ligi ya nchi 20 kila moja, kama tunavyoona kwenye mpira, huku kuwa kwenye ligi kuu ni kuwa ishirini bora kwa misingi ya Kipimo cha Maendeleo ya Binadamu, tungepata taswira nzuri.

Mwaka 2019, hakuna nchi barani Afrika ambayo ingekuwa kwenye ligi 3 kuu. Mauritius ndiyo nchi pekee katika bara hili ambayo ingekuwa katika ligi ya 4. Upande mwingine, Mali, Burundi, Sudan Kusini, Chad, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Naija zingekuwa katika ligi ya chini zaidi, ligi ya 10.

Kutokana na takwimu za miongo iliyopita kama ilivyoelezewa hapo juu, si vigumu kuona kiwango cha changamoto ambazo bara hili linakumbana nazo ili kuweza kufikia katika ligi za juu za uchumi wa dunia.

Ingawa kuna hatua kadhaa zinazoweza kuchukuliwa, mapendekezo matatu hapa chini yanaweza kutoa nafasi ya kukabiliana na changamoto hizi:

  1. Ni muhimu kwa wadau wa nyanja za maendeleo kubadili itikadi zao

Ni muhimu kwa wadau katika nyanja za maendeleo, yaani, serikali, biashara na wananchi kukubali kuwa kuna mapungufu ya maendeleo na kuhakikishiwa kwamba kukabiliana nazo kutamnufaisha kila mtu, hata kama anaishi kwenye bara hili au la.

Katika kutimiza majukumu yao, kila mtaalamu anaweza kujiuliza maswali mepesi: je, tunaliwezeshaje bara hili kutatua mapungufu yake ya maendeleo? Ni nini tunachoweza kufanya kwa njia tofauti ili kukabiliana na mapungufu ya maendeleo tunapotekeleza majukumu yetu?

  1. Kujiimarisha baada ya Uviko-19

Nchi nyingi ziliweka vikwazo kama njia za kudhibiti kusambaa kwa tandavu hii, kama vile kufunga shule na biashara. Miaka miwili baadaye, nchi nyingi zinajifunza kuishi na virusi hivi na zimeondoa au ziko katika mchakato wa kuondoa vikwazo hivi na kufungua uchumi wao kikamilifu.

Serikali za Afrika ni lazima ziweke kipaumbele kwenye uvumbuzi na mielekeo ya maendeleo itakayowapa watu kipaumbele katika kujenga upya mifumo ya uchumi ili kusaidia urejesho wa haraka. Hii inajumuisha kutumia teknolojia ya kidijitali ambayo matumizi yake yaliimarika zaidi wakati wa tandavu na urejesho wa kimazingira ambao ni nguzo muhimu ya Ajenda ya 2030 kwa maendeleo endelevu inayolenga kuilinda sayari hii.

  1. Kutumia Ajenda 2030 ili Kuimarisha Maendeleo Endelevu

Ajenda ya 2030 ni mfumo wa mageuzi na mbinu ya uwajibikaji - kuendeleza malengo ya maendeleo endelevu pia kutawezesha bara hili kufikia maazimio yake ya 2063 ya Afrika tunayoitaka. Afrika inaweza kunufaika zaidi na mifumo ya maendeleo kwa kufanya sehemu nyingi za dunia kuwajibika kuchukua au kutochukua hatua.

Bila shaka, hii inamaanisha Afrika pia inapaswa kuchukua nafasi yake - kupitia hatua za maendeleo na uwekezaji - ili kuweka sauti yake katika mbinu hii ya kimataifa kwa ajili ya mageuzi na uwajibikaji.

Hatua hizi tatu, ingawa kamili, zinaweza kuwezesha wadau katika nyanja za maendeleo kukubali mapungufu ya maendeleo ya Afrika. Mapungufu haya ni ya kina kuliko ambavyo wengi wanaweza kuamini na kuyakabili kutanufaisha kila mtu.? Pia yanaondoa dhana kwamba kuna mtu tofauti ambaye anawajibika, kila mtu anaweza kufanya kitu.

Kila mwafrika anahitaji kujiuliza anaweza kufanya nini zaidi katika kiwango chake ili kukabiliana na mapungufu ya maendeleo.

Zaidi ya hayo, ili kutumia mikakati ya urejesho baada ya Uviko-19, Ajenda ya 2030 kwa Maendeleo Endelevu na Ajenda ya Afrika ya 2063 kama fursa inapaswa kuwapa watu kipaumbele katika ujenzi upya na bora.


Bw. Mugisha ni Mshauri wa ushirikiano wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG) katika Kituo cha Huduma cha Kikanda cha UNDP Barani Afrika.

More from this author