Kuisaka mizizi ya familia zaidi ya DNA

Get monthly
e-newsletter

Kuisaka mizizi ya familia zaidi ya DNA

Wataalam watatu wa unasaba wanavifafanua vikwazo na mafanikio katika kutafiti ukoo wa Wamarekani Waafrika
Afrika Upya: 
18 January 2024
Photos of Dena M. Chasten (on the beach)
Dena M. Chasten (supplied)
Dena M. Chasten amesimama ufukweni. Alipata wazazi wake waliomzaa na sasa anafanya kazi kama mtaalamu wa nasaba akiwasaidia Waamerika wengine wa Kiafrika katika kurekebisha matawi yaliyovunjika ya miti ya familia zao.

Akiwa mtoto wakupangwa, Dena M. Chasten mara nyingi alihisi kutengwa na familia yake. Hisia hiyo inahusiana natajriba yakeya kuwa MmarekaniMwafrika huko Marekani. Kila maraaliwazia alikotoka na alikostahili.

"Tofauti nikwambaanapokuwa umepangwa, kwakiasi kikubwa, huwa unatakiwa. Nilikuwa na bahati sana kwamba familia nzuri ilinilea,” alisema mzaliwa huyo wa Philadelphia. “Hata nilifanana nao, lakini nilijua kabisa kwamba hatukuwa na uhusianowa kinasabai. Bado nilijihisi nimepotea.”

Tajriba hiyoilimtia moyo Bi. Chasten sio tukuwasaka wazazi wakekibayolojia bali pia kuuchunguza ukoo wake. Alianza uchunguzi wa kinasaba na ukoo ambaouliyazua maswali mengi kuliko majibu.

Katika eneo lote la katikati mwa Atlantiki, Bi. Chasten ameshiriki safari yake katika maktaba, jamii za kihistoria na hata katika huko Washington, DC.

Kwa kuwa sasa amewapata wazazi wake waliomzaa, anafanya kazi kama mtaalamu waunasaba, akiwasaidiaWamarekani Waafrika wengine katikakuurekebishauhusiano wao wa kinasaba uliovunjika.

Ushahidi wa stakabadhi

"Mfumo wa utumwaulizitenga familia, lakini DNAhuziunganisha familia hizo," alisema Nicka Sewell-Smith, mtayarishaji mkuu wa hadithi wa .

Nicka Sewell-Smith
Mfumo wa utumwa ulizitenga familia, lakini DNA iunaziunganisha famila hizo.
Nicka Sewell-Smith
Mzalishaji Mkuu wa Hadithi, Ancestry.com

Watu hawapaswi kutegemea tu DNA (Asidi DeoksiriboNukleini), alisema. "Wale ambao tumezamakatika taaluma ya unasaba tunataka kupata ushahidi wa stakabadhiilikuifanya miunganisho hiyo.”

Kwenye makala ya Finding Your Roots na Henry Louis Gates Jr., watazamaji wanawafuatilia Wamarekani Waafrika wengi huku wakisaka ukoo wao hadi kwa mababu zao waliokuwa watumwa.

“"Wamarekani Waafrika walikabiliwa na kikwazo cha kipekee cha kinasaba katika miaka hiyo 10 hadi 20 ya kwanza kutoka utumwani na Vita vya Wenyewe kwa Wenyewe," Nick Sheedy, mtaalamu mkuu wa unasaba katika kipindi hicho.“"Sensa ya 1870 ni sensa ya kwanza yakitaifa ambayo ilimworodhesha kila mtu kwa jina," Bw. Sheedy aliiambia Africa Renewal katika mahojiano, akiongeza kuwa majina hayoyangebadilikakutegemea umiliki, uchaguzi wa kibinafsi na sababunyinginezisizoweza kuelezeka.

Kufuatilia mizizi ya Waafrika waliokuwa watumwa, ambao walichukuliwa kuwa mali, kwa kawaida kulihitaji kuangalia mauzo ya mirathi, rekodi za mirathi, hati za kodi na hatimiliki, Bw. Sheedy alieleza. Wakati wa Vita vyaWenyewe kwaWenyewe, aliongeza, askari walizichoma mahakama za kaunti ambazo zilikuwa na kumbukumbu nyingi za enzi ya watumwa.

"Hakuna orodha kuu ya Waafrika waliofanywa watumwa," alisema Bi. Sewell-Smith.

Ingawa rekodi nyingi haziko mtandaoni, alibainisha kuwa hati milioni 3.5 kutoka —ambazosasa zinapatikana kwenye Ancestry.com — ni mahali pazuri pa kuanzia.

Mojawapo yamafanikio yaushahidi wa stakabadhi wa Bw. Sheedyyalihusiana na Ahmir "Questlove" Thompson, mpiga ngoma kutoka bendi ya hip-hop inayoitwa The Roots.

"Tuligundua kuwa mababu zake walikuja kwenye Clotilda," Bw.Sheedyalisema. Ilikuwa meli ya mwisho inayojulikana ya watumwa kuwasili Marekani.”

Nick Sheedy, Lead Genealogist, Finding Your Roots with Henry Louis Gates, Jr.
Sote tunahusiana.
Nick Sheedy
Mtaalam Mkuu wa Unasaba, Finding Your Roots with Henry Louis Gates, Jr.

Ulinganifu waDNA

Bi. Sewell-Smith anapoufichua ukoo wake mwenyewe, hafuatilii asili yake katika nchi moja ya Kiafrika;anaandama bara zima. "NiLazimauzingatie ni vizazi vingapi vilikuwepo tangu kupiga marufuku mwaka 1808 kwa uingizaji wa watumwa kutoka Afrika," alisema.

Kuhesabu vizazi sita kurudi nyumakunahusisha kufuatilia mizizi yamababu namababu 64 kutokamaeneo mbalimbaliya Afrika.

Bi. Sewell-Smith anaonya kwamba watu hukosa uhakika ikiwa wanazingatia nchi au asilimia. "Kwa Wamarekani Waafrika, asili zetu zote za Kusini mwa Jangwa la Sahara zinatoka katika maeneo mengi," alisema. “Ninajua ‘wapi’ . Ninataka kujua ‘nani’.”

Katika familia ya Bi. Sewell-Smith, "nani" ni pamoja na bibi yake mwenye umri wa miaka 99, ambaye babu na babu walikuwa watumwa.

"Bibi yangu anashiriki 30 centimorgans za DNA na mwanamke wa Naijeria ambaye ni kizazi cha kwanza katika familia yake kuzaliwaMarekani," alisema. "Huyo ni binamu wa nne!"

Watu wanaufanya uvumbuzi huu kila siku, alisema.

HataBw. Sheedy anawezakuipata mizizi yakekatika bara hilo. “Bibi yangu, Betty alikuwa mweupehasa na nywele za kimanjano na macho ya buluu.Mababu zake wote walikuwa waanzilishi wa California, naalikuwa na karibu asilimia tatu ya DNA ya Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara," alisema. "Sote tunahusiana."

Wataalamu wa unasaba wanaweza kutatua mafumbo zaidi ikiwa watu wengi watapima DNA, alisema Bi. Sewell-Smith.

"Uwezoukokwenye ulinganifu wa DNA," aliongeza. Hiyo ndiyo itasimulia hadithi, kutupa vidokezo, kututuma kwenyehifadhi za nyaraka na kutuunganisha na watu ambao hatungejua kuwa walikuwa jamaa zetu.

Binamu wa mbali

Huku akisubiri matokeo ya vipimo kadhaa vya DNA, Bi Chasten alisema anatarajia kubaini mahali ambapo angeweza kuwakilisha. "Nilikuwaninaenda kutafuta nchi yangu na kuwa na uhusiano wangu."

Dena M. Chasten, genealogist
You can’t depend just on the DNA. You have to do the research.
Dena M. Chasten
mtaalam wa unasaba

Badala yake ulifichua kwamba babu yake mkubwa wakuukeni alikuwa mwanamke wa Ulaya, nauchunguzi wake wa kiautosom ulionyesha asilimia ya DNA kutokakanda za pande zote nne kuu za bara hilo.

Akiwaamestaajabu na kuchanganyikiwa, Bi. Chasten alisema alikuwa na maswali zaidi kuliko hapo awali. Wakati huu, hata hivyo, alijuaniwapi pa kuangalia. "Huwezi kutegemea tu DNA," alisema. "Ni lazima uufanyeuchunguzi, ili yote yawe na maana."

Bi. Chasten aliupata ulinganifu thabitiwa DNA nchini Ghana, nchi iliyobeba asilimia zake kubwa zaidi. Aliwasiliana na binamu huyu wa mbali na akasikia hadithi ambayo ingali inampamsisismko.

"Kulikuwa namighani kwamba nyanya yake [binamu wa Ghana] angenda kulala kila mara akiomba msamaha kwa sababu alijua jukumu lamababuzake katika biashara ya utumwa," Bi. Chasten alisema. "Kilikuwa kitu ambacho alihitaji kulipia."

Hadithi hiyo iliibua hisia zinazokinzana kwa Bi. Chasten: hangewezakuyakubali matendo yamababuzake alipokuwa akimfariji binamu yake.

“Nilimwambia, ‘Usijali kuhusu hilo.Tunarejea. Siwezi kueleza kilichotokea wakati huo, lakini sasa tuyanarekebisha.’ Kwa hiyo wengi wetutunarejea nyumbani.”

Bi.Chasten alilizuru bara hilo kwa mara ya kwanza mwishoni mwa mwaka jana.