缅北禁地

Bunge kutotekeleza mapendekezo ya ripoti ni jambo la kusikitisha- Profesa Assad

Get monthly
e-newsletter

Bunge kutotekeleza mapendekezo ya ripoti ni jambo la kusikitisha- Profesa Assad

缅北禁地News
Profesa Musa Juma Assad ambaye ni mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali nchini Tanzania, wakati wa mahojiano na Idhaa ya Kiswahili. Picha: 缅北禁地News/Assumpta Massoi
Picha: 缅北禁地News/Assumpta Massoi. Profesa Musa Juma Assad ambaye ni mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali nchini Tanzania, wakati wa mahojiano na Idhaa ya Kiswahili
Picha: 缅北禁地News/Assumpta Massoi. Profesa Musa Juma Assad ambaye ni mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali nchini Tanzania, wakati wa mahojiano na Idhaa ya Kiswahili

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali nchini Tanzania, CAG Profesa Musa Assad amezungumzia kitendo cha baadhi听 ya ripoti zinazoonyesha听 ubadhirifu kutoshughulikia ipasavyo na Bunge la nchi hiyo. Taarifa zaidi na Arnold Kayanda.

Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi nchini Tanzania kila mwaka hukabidhi ripoti zake za ukaguzi wa taasisi za umma ambazo pamoja na kuonyesha matumizi ya fedha pia hutoa mapendekezo.

Hata hivyo kumekuwepo na shaka shuku kutokana na kitendo cha baadhi ya mapendekezo kutotekelezwa ambapo katika kusaka ufafanuzi nilizungumza hivi karibuni na Profesa Musa Assad, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali Tanzania wakati akiwa New York, Marekani na kumuuliza kulikoni hayatekelezwi?

鈥淪asa hilo ni jambo ambalo kimsingi ni kazi ya Bunge. Kama tuantoa ripoti inaona kuna ubadhirifu na hatua hazichukuliwi huo kwangu mimi ni udhaifu wa Bunge. Bunge linatakiwa lisimamie na lihakikishe kwamba pahali penye matatizo basi hatua zinachukuliwa. Sisi kazi yetu ni kutoa ripoti tu. Na huo udhaifu nafikiri ni jambo la kusikitisha, lakini ni jambo ambalo tunaamini muda si mrefu huenda litarekebishika.鈥

Na je tatizo ni nini?

鈥淭atizo kubwa tunahisi kwamba Bunge linashindwa kufanya kazi yake kama inavyotakiwa.Na sitaki kuwa labda nasema jambo hili kwa sababu linahusisha watu fulani, hapana ni kwamba Bunge likifanya kazi yake vizuri hata udhaifu ambao unaonekana utakwisha kabisa.鈥