缅北禁地

Mahitaji ya kuwatafutia wakimbizi nchi ya tatu yalifikiwa kwa chini ya asimilia 5 tu duniani kote.

Get monthly
e-newsletter

Mahitaji ya kuwatafutia wakimbizi nchi ya tatu yalifikiwa kwa chini ya asimilia 5 tu duniani kote.

缅北禁地News
Prise Josphine na Jemima Nsenga ni wakimbizi waliohamia nchi ya tatu Marekani, waliposhiriki hafla ya kukaribisha kupitishwa kwa mkata wa wakimbizi kwenye Umoja wa Mataifa. Picha: 缅北禁地News/Grece Kaneiya
Picha: 缅北禁地News/Grece Kaneiya. Prise Josphine na Jemima Nsenga ni wakimbizi waliohamia nchi ya tatu Marekani, waliposhiriki hafla ya kukaribisha kupitishwa kwa mkata wa wakimbizi kwenye Umoja wa Mataifa.
Picha: 缅北禁地News/Grece Kaneiya. Prise Josphine na Jemima Nsenga ni wakimbizi waliohamia nchi ya tatu Marekani, waliposhiriki hafla ya kukaribisha kupitishwa kwa mkata wa wakimbizi kwenye Umoja wa Mataifa.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesema mwaka jana 2018 mahitaji ya kuwapatia wakimbizi nchi ya tatu ya hifadhi yalikuwa ni chini ya asilimia 5 licha ya kwamba mwaka huo ulivunja rekodi ya idadi ya kubwa ya wakimbizi waliosaka hifadhi ya nchi ya tatu.听听

Takwimu za UNHCR zilizotolewa leo huko mjini Geneva, Uswis听zinafafanua kuwa takribani wakimbizi milioni 1.2 waliohitaji听kuhamishiwa nchi nyingine kwa mwaka 2018, ni wakimbizi 55,692 pekee ambao walipatiwa makazi mapya.

Idadi kubwa zaidi ya wakimbizi hao waliosaka hifadhi nchi ya tatu kwa msaada wa UNHCR ni听walitoka nchi zenye wakimbizi wengi zaidi ikiwemo Lebanon wakimbizi听9,800, Uturuki wakimbizi听9,000, Jordan wakimbizi听5,100听na Uganda wakimbizi听4,000.

Akifafanua zaidi, Shabia Mantoo ambaye ni msemaji wa UNHCR mjini Geneva, Uswisi amesema,"Asilimia 68 ya majina yaliyowasilishwa mwaka jana walikuwa manusura wa vurugu na mateso, wale wanaohitaji kulindwa kisheria听 na wanawake na wasichana waliko hatarini. Zaidi ya nusu yaani asilimia 52 ya maombi ya kutafutiwa nchi ya tatu walikuwa watoto鈥

Kwa mujibu wa UNHCR, katika mwaka huu wa 2019, inakadiriwa kuwa wakimbizi milioni 1.4 ambao wanaishi katika nchi 65 duniani kote watahitaji kuhamishiwa katika nchi ya tatu.

Bi. Mantoo amesema wakimbizi wengi ambao wanatakiwa kuhamishwa ni pamoja na wakimbizi wa Syria ambao kwa sasa wanahifadhiwa katika nchi mbalimbali za mashariki ya kati na Uturuki kwa hiyo,听鈥淢kataba wa kimataifa kuhusu wakimbi unatoa wito kwa mataifa mbalimbali kutoa nafasi zaidi za kuwapokea wakimbizi kwa kupanua programu zilizoko hivi sasa au kwa kuanzisha programu mpya鈥