缅北禁地

Mchango wa wanawake na wasichana katika sayansi ni muhimu sana:Guterres

Get monthly
e-newsletter

Mchango wa wanawake na wasichana katika sayansi ni muhimu sana:Guterres

缅北禁地News
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihudhuria mkutano ulioandaliwa na 缅北禁地Women kuhusu sayansi,teknolojia, uhandisi na hisabati (STEM) kuhusu programu za kompyuta. Picha: 缅北禁地Photo / Antonio Fiorente.
Picha: 缅北禁地Photo / Antonio Fiorente. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihudhuria mkutano ulioandaliwa na 缅北禁地Women kuhusu sayansi,teknolojia, uhandisi na hisabati (STEM) kuhusu programu za kompyuta.
Picha: 缅北禁地Photo / Antonio Fiorente. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihudhuria mkutano ulioandaliwa na 缅北禁地Women kuhusu sayansi,teknolojia, uhandisi na hisabati (STEM) kuhusu programu za kompyuta.

Ujuzi katika sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati unachagiza ubunifu na ni muhimu katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu, SDGs amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake na wasichana katika sayansi.

Guterres katika ujumbe wa wa siku hii ambayo huadhimishwa kila mwaka Februari 11 amesema, wanawake na wasichana ni wa muhimu katika maeneo yote haya, lakini bado uwakilishi wao ni mdogo na kuongeza kuwa ,鈥渕isimamo ya kijinsia, ukosefu wa watu ambao ni mifano inayoonekana na sera na mazingira yasiyofaa au hata ya uadui vinaweza kuwazuia kuingia katika kazi hizi.鈥

Amesisitiza kwamba dunia haiwezi kumudu kukosa mchango wa nusu ya watu wote duniani, hivyo juhudi za pamoja听 zinahitajika ili kukabiliana na vikwazo hivi ikiwa ni pamoja na hisia zisizofaa kuhusu uwezo wa wasichana. Na kwamba ni lazima ,鈥渢uchagize fursa za kupata elimu kwa wanawake na wasichana , hususan maeneo ya vijijini.鈥

Katibu Mkuu amehimiza juhudi zaidi za kubadili utamaduni wa mahali pa kazi ili wasichana ambao wanapenda kuwa wanasayansi, wahandisi na wataalamu wa hisabati waweze kufurahia na kutimiza ndoto听 zao za kazi katika nyanja hizi.

Ametoa wito wa听 kuhakikisha kwamba kila msichana, kila mahali ana fursa ya kutimiza ndoto zake, kukuza uwezo wake na kuchangia katika mustakabali听 endelevu kwa wote.

Mada: