Katika wapiganaji wapatao 600 wa UFC duniani, 11 ni Waafrika.
Wanajumuisha wale wa uzani wa wastani kwa sasa na mabingwa wa uzani wastani.
Ìý
2019 ulikuwa mwaka wa kufana kwa Israel Adesanya mwenye umri wa miaka 30. Adesanya alizaliwa Lagos, Nijeria na kulelewa New Zealand tangu alipokuwa na umri wa miaka 12. Amekuwa bingwa wa uzani wa kati katika mashindano ya kilele ya mapigano (UFC), mwendelezaji maarufu sana duniani wa Sanaa Mseto ya Kijeshi (MMA), akiwa na wapiganaji mbalimbali kutoka makundi tofauti ya uzani.
MMA inaruhusu wapiganaji kutumia mtindo wowote wa kupigana, kama vile ndondi, mieleka, au kufyatua ndondi mtindo wa Thai,Ìý nayo UFC inaunda uwiano katika kundi za uzani.
Upiganaji wa kawaida unajumuisha raundi tatu za dakika 5 (raundi tano za dakika 5 kwa upiganaji wa mashindano), pale ambapo kila mpiganaji anakuwa na fursa ya kumshinda mpinzani wake, kama ilivyo katika ndondi. Ikiwa hakuna mshindi wa wazi baada ya muda uliowekwa,Ìý majaji watatu huamua mshindi.
Licha ya uwakilishi wa dunia nzima wa wapiganaji, kuna wapiganaji wa UFC 11 pekee wazaliwa wa Afrika kutoka 580 walioajiriwa na UFC. Adesanya alinyakua taji la mashindano ya uzani wa kati huku akimshinda Kelvin Gastelum (Mmarekani) na Robert Whittaker (Kutoka Australia) katika mapigano yaliyofuatana.
Adesanya: ‘The Last Stylebender’
Adesanya hakuanza mafunzo kikamilifu hadi alipotimia miaka 21, alipohamia Auckland kujiunga na timu ya City Kickboxing. Anasema kuwa mapambano yake na uonevu, upweke na ubaguzi wa rangi yalimchochea kufuata michezo ya kijeshi.
Katika kuanza kazi yake ya kitaaluma, Adesanya alishindana katika ndondi na mateke, ndondi, na MMA, alipojilimbikizia rekodi (kushinda na kushindwa) ya 75-5, 5-1, na 11-0, mtawaliwa, kabla ya kujiunga na UFC mapema 2018, ambapo anasalia bingwa, akishinda mapigano manane kamili.
Anajulikana kamaÌý ‘the Last Stylebender’ kwa mazoea yake ya mazoezi kabla ya kupigana. Amenyakua marupurupu saba yanayohusiana na mashindano, ikijumuisha 'mapigano ya mwaka' 2019. Kwa maneno yake, anasema ''nilirudisha dhahabu Afrika.''
Adesanya amemshinikiza rais wa UFC kuleta mashindano Afrika kuimarisha umaarufu wa MMA na kuunda ajira barani.
Francis Ngannou: ‘The Predator’
Kama ilivyo katika michezo mingine, COVID-19 imesitisha UFC. Baada ya kusimamishwa kwa miezi miwili, imekuwa moja ya michezo michache ya kitaalamu kuanza tena haraka mwezi Mei, ingawa ukiwa na wafanyakazi wachache na bila kuwa na mashabiki kushuhudia.
Francis Ngannou, Mfaransa kutoka Kameroon, ni mmoja kati ya wachache walioshiriki katika mashindano ya baada ya COVID-19. Ngannou aliyekulia Batie, magharibi mwa Kameroon,Ìý alikuwa akifanya kazi katika machimbo ya changarawe tangu akiwa na umri mdogo wa miaka 13 ili kusaidia familia yake.
Akiwa na umri wa miaka 26,Ìý alihamia Paris kuendelea na mchezo wa ndondi. Ngannou alikosa makao huko Paris hadi rafiki fulani mahali alipokuwa akifanya kazi katika makazi ya wasio na makao, alipomhimiza kujaribu MMA. Alianza kazi yake ya kitaalamu mwaka mmoja baadaye, wakati baadhi ya wapiganaji wakiwa na tajriba ya mwongo mmoja.
Tangu alipojiunga na UFC mnamo Desemba 2015, Ngannou ameshinda mashindano 10 na kupoteza 2 (10-2) katika kundi la uzani mzito baada ya mwanzo wa taaluma wa 5-1. Ingawa alishindwa katika fursa yake ya kwanza ya kutafuta taji, Ngannou atapata fursa nyingine hivi karibuni.
Kuwiana na jina lake la utani, ‘the Predator,’ lililochochewa na filamu inayoongozwa naÌý Arnold Schwarzenegger,Ìý kwa jina kama hilo, Ngannou ameshinda mapigano 15, (mpinzani kushindwa kuendelea, mchezo kusitishwa na refa au mpinzani kujisalimisha), ushindi ukitokea katika raundi ya kwanza katika mashindano 11.
Ngannou aliwekwa karantini wakati wa mapigano yake ya Mei 9, alipimwa mara kadhaa na kupigana katika ukumbi usiokuwa na mashabiki. Kuhusu usumbufu wa upimaji wa kutumia sampuli ya puani, alisema, ''afadhali nipigwe ngumi.''
Pamoja na ufanisi wake michezoni, Ngannou hajasahau asili yake. Ameanzisha shirika lisilo la kiserikali la Wakfu wa Francis Ngannou nyumbani kwao Kameroon, wakfu ambao ''unalenga kuwawezesha vijana wa Kameroon ili kuyaboresha maisha yao.''Ìý Wakfu huu umesaidia kutayarisha chumba cha mazoezi ambapo vijana hufanya mazoezi na kufuatilia MMA, huku Ngannou akizuru kila mara na kusaidia mwenyewe.
Kamaru Usman: ‘The Nigerian Nightmare’
Mpiganaji mwingine kutoka Nijeria, bingwa wa uzani wastani na rafiki yake Adesanya, ni Kamaru Usman mwenye umri wa miaka 33. Usman alizaliwa Auchi, kusini mwa Nijeria. Alihamia Marekani alipokuwa na umri wa miaka minane na baadaye akajuhusisha na mchezo wa mieleka, na akapata ufanisi alipokuwa katika shule ya upili na chuo.
Huku akifanya mazoezi kwa Michezo ya Olimpiki ya 2012 na kufanya kazi kamaÌý mkufunzi wa mapigano, Usman alitaka kufuatilia taaluma yenye faida kubwa na akageukia MMA, hatimaye akajiunga na UFC.
Tangu michezo yake ya kwanza mwaka 2015, Usman amethibitisha kutositishwa, huku akishinda mapigano 11, na kumshinda Tyron Woodley (Mmarekani) na kuwa bingwa wa uzani wastani na bingwa wa kwanza Mwafrika mnamo Machi 2019.Ìý
Usman ameendeleza jina lake ‘the Nigerian Nightmare,’ lililochochewa na Nyota wa zamani wa Ligi ya Kitaifa ya Kandanda ya Marekani (NFL), Christian Okoye ambaye alijulikana kwa jina hilo na ambaye alimpa Usman idhini ya kulitumia.
Kama Adesanya, Usman ametetea mashindo ya UFC kuletwa Afrika kama njia ya kushirikisha vijana. Ingawa COVID-19 huenda imechelewesha uwezekano wa UFC kufanyika Afrika, wapiganaji hawa wanaendelea kushinda na kuthibitisha nguvu ya Afrika ukumbini.
Huku mashindano ya UFC yakihamia Abu DhabiÌý katika Falme za Umoja wa Kiarabu kutokana na kulegezwa kwa vikwazo vya usafiri, Kamaru Usman amepangiwa kutetea taji lake kwa mara ya pili mnamo July 11.