Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema wakati dunia ikipambana na janga la mlipuko wa听COVIDI-19, changamoto kubwa kabisa kuwahi kuikabili dunia tangu vita vya pili vya dunia, kunashuhudiwa pia mlipuko mwingine wa hatari, ambao ni mlipuko wa taarifa potofu
Kupitia ujumbe wake alioutoa leo kupitia mtandao Guterres amesema听鈥淒uniani kote watu wanaogopa, wanataka kujua nini cha kufanya na wapi pa kukimbilia kupata ushauri.听Huu ni wakati wa sayansi na mshikamano.听Lakini bado mlipuko wa taarifa potofu unasambaa duniani kote.鈥
Ameongeza kuwa ushauri wa afya wenye madhara na nukuu za hatari kama mafuta ya nyoka vinazidi kuongezeka.
Taarifa za uongo imekuwa ndio wimbo
Katibu mkuu ameonya kwamba听鈥Uongo ndio unaotawala hewani, nadharia potofu zimeghubika na kuathiri mtandao huku Chuki ikishika kasi, unyanyapaa na kuwanyanyasa watu na vikundi nako kunaongezeka.鈥
Amehimiza kwamba huu ni wakati ambapo dunia inapaswa kuungana dhidi ya ugonjwa huu wa taarifa potofu pia na kusema听鈥淐hanjo yake ni uaminifu, kwanza uaminifu katika sayansi.鈥
听Pia amewapongeza waandishi wa Habari na wengine ambao wanakagua ukweli wa mlima wa taarifa potofu na machapisho kwenye mitandao ya kijamii.
Wamiliki wanajibika pia
听Bwana Guterres ameyageukiwa makampuni ya mitandao ya kijamii na kusema听鈥測anapaswa kufanya juhudi zaidi kukata mizizi ya chuki na dhana potofu kuhusu COVID-19.听Pili uaminifu katika taasisi zilizowekwa katika kuchukua hatua, kuwajibika, utawala na uongozi wenye msingi wa ushahidi.鈥
Na ametaka pia kuwe na imani听听miongoni mwa watu akisema听听kuheshimiana na kudumisha haki za binadamu lazima kuwe ni dira yetu katika kukabilianana mgogoro huu.
听"Kwa Pamoja hebu tuukane uongo na upuuzi uliotawala huko nje.鈥
听Mkakati kukabili taarifa potofu
Leo hii Katibu mkuu听听ametangaza mkakati mpya wa mawasiliano wa Umoja wa Mataifa ambao amesema utajaza mtandao kwa taarifa sahihi na sayansi huku ukikabiliana na ongezoko la taarifa potofu,ambazo ni sumu inayoweka maisha katika hatari zaidi.
鈥淜wa sababu ya Pamoja, kutumia ufahamu na ukweli tunaweza kuishinda COVID-19 na kujenga dunia yenye usawa, haki na mnepo.鈥 Amehitimisha Bwana. Guterres.