Jamii msiwe na hofu ya kuchangia damu wakati huu wa COVID-19, bado tunahitaji kuokoa maisha -Dkt Kitundya

Get monthly
e-newsletter

Jamii msiwe na hofu ya kuchangia damu wakati huu wa COVID-19, bado tunahitaji kuokoa maisha -Dkt Kitundya

山News
14 May 2020
By: 
Dkt. Leah Kundya, Mkuu wa kitengo cha Damu Salama, hospitali ya rufaa ya Dodoma nchini Tanzania.
山News Kiswahili
Dkt. Leah Kundya, Mkuu wa kitengo cha Damu Salama, hospitali ya rufaa ya Dodoma nchini Tanzania.

Kitengo cha damu salama katika hospitali ya rufaa mkoa wa Dodoma nchini Tanzania kimewatoa hofu wachangiaji wa damu kuwa uwepo wa ugonjwa wa virusi vya Corona auCOVID-19usiwatishe kwenda kuchangia damu kwani hawawezi kuambukizwa wala kuwaambukiza wengine kwa kuchangia damu.

Msimamizi wa kitengo hicho Dkt. Leah Kitundya anasema kwa sasa kiwango cha uchangiaji wa damu kimepungua kwa sababu wachangiaji wakubwa ni wanafunzi wa sekondari na vyuo ambao wamerudi nyumbani baada ya masomo kusitishwa kwa lengo la kuepuka msongamano unaoweza kuchangia maambukizi mapya ya virusi hivyo wakishirikiana na wanajeshi.

Dkt. Leah akaongeza kuwa changamoto ya virusi vya Corona vimeathiri kwa kiasi kikubwa uchangiaji wa damu na kusababisha kutofikia lengo walilojiwekea la kila mwezi kukusanya chupa 1000 hadi 1500 lakini sasa hali imekuwa tofauti ambapo kwa mwezi uliopita wamekusanya chupa 500 akisema kuwa mwitiko wa wananchi kujitokeza kuchangia ni mdogo.

Amesema kuwa,"jamii haina mwamko wa kuchangia damu, mwezi uliopita tulipata chupa za damu 558 kiasi kwamba tumerudi nyuma sana. Kipindi cha nyuma kwa mwezi tulikuwa tunakusanya chupa 800 hadi 900 lakini mwezi uliopita tumekusanya chupa 500 tu. Kwa hivyo tumerudi nyuma sana.Kwa hio sasa basi tukisema hatuchangii damu kwa sababu ya corona tunasema wenzetu ambao wamelala hospitalini wapoteze maisha. Ni nani anayetakiwa kuchangia damu?Ni mimi na wewe ilimradi tu uwe na umri wa kuanzia miaka 18 hadi 65. Uzito kilo 50 kwenda juu,usiwe na magonjwa sugu kama kuanguka kifafa ,magonjwa ya moyo,ugonjwa wa kisukari ugonjwa wa pumu na usiwe mama mnyonyeshaji mtoto wa chini ya miezi sita au mama mwenye hali ya ujauzito."

Dkt. Leah amesema hata hivyo kuwa wanachukua tahadhari wakati wa uchangiaji wa damu katiki kipindi hiki cha maambukizi ya virusi vya Corona.

Kuhusu suala ya kwamba ukichangia damu unatapa ugonjwa wa Corona, Dkt. Leah amesema,"lakini kuchangia damu sio eti ile damu yaweza kuambukiza mtu kupata corona apana! kunafanya kazi tukichukuwa usalama ilikuzuia watu wasipate maambukizi ya Corona."

Pia msimamizi huyo akatoa ufafanuzi juu ya malalamiko ambayo hutolewa na baadhi ya watu kuwa wamekuwa wakitozwa fedha kupata damu kwa ajili ya wagonjwa wao akisema kuwa,"kulipia sio kulipia kwa hela uchangiaji wa hiari unakuwa mwanachama na unapata kadi siku ambayo utakuwa mgonjwa unaambiwa hakuna kulipia hiyo damu ya kulipia kwa maana ya kurudisha sio kwa kuchangia hela."