Kemikali za sumu kwenye mazao ni ‘mwiba’ kwa asali bora

Get monthly
e-newsletter

Kemikali za sumu kwenye mazao ni ‘mwiba’ kwa asali bora

山News
20 May 2020
By: 
Nyuki ni wadudu muhimu sana, bila uwepo wao maua hayatachavuliwa na upatikanaji wa chakula utakuwa hatarini.
FAO
Nyuki ni wadudu muhimu sana, bila uwepo wao maua hayatachavuliwa na upatikanaji wa chakula utakuwa hatarini.

Kuelekea siku ya nyuki duniani kesho tarehe 20 mwezi Mei, wafugaji wa nyuki nchini Tanzania wamezungumzia umuhimu wa wakulima kuepuka kutumia kemikali za sumu ili kuhakikisha asali ya nyuki haina madhara yoyote kwa afya ya binadamu.

Frederick Katulanda ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa waandishi wa habari wa ufugaji nyuki wilaya ya Misungwi, mkoani Mwanza, amesema hayo akihojiwa na kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa, UNIC Dar es salaam, akieleza kuwa hiyo ni moja ya changamoto wanazopata kwenye ufugaji.

Lichaya asali, mazao mengine ya nyuki ambayo tunaweza kuyachakata ni nta na tunaichakata kwa kutengeneza mishumaa pekee yake, lakini matumizi mengine kama kutengenezagundi,kutengeneza dawa ya kunga'rishia viatu, kutengeneza pengine mafuta au sabuni na manukato kwa ajili ya hizi nta bado hatujafikia. Kwahivyo iwapo watu wengi watajitokezaviwanda vingi vya kuchakata mazao ya asali basi kuna uwezekano mkubwa wa kuongeza ajiranyingikupitia sekta hii ya asali nakulileteataifa mapato makubwa sana

Bwana Katulanda akaenda mbali zaidi kutoa wito kwa wawekezaji hususan katika kuwezesha kunufaika zaidi na mazao ya asali akisema kuwa,

Hizi dawazinaathirisana ukuaji wa nyuki lakini pia zinasababisha sisi wavunaji wa asali tupate asali ambayo haifai katika soko la kimataifa kwasababu unapolima kwa mfano nyanya au pamba unapulizia dawa nyuki wanakwenda kuchukua yale maua kwa ajili ya kupata poleni au poleni ikiwa na viambato vyasumusasa hii poleninyuki wanaitumiakutengenezea asali na kama watachukua poleni ambayo maua yake yamepuliziwa dawa maana yake ni kwamba tutazalisha asali yenye dawa na itakuwa ni asali isiyofaa kwa matumizi ya binadamu