Kutoka kutumikishwa vitani Sudan Kusini hadi kumiliki karakana ya samani

Get monthly
e-newsletter

Kutoka kutumikishwa vitani Sudan Kusini hadi kumiliki karakana ya samani

山News
30 April 2020
By: 
Malis, (si jina lake halisi) akiwa kwenye karakana yake kwenye eneo la Yambio jimboni Equatoria Magharibi nchini Sudan Kusini.
UNMISS/Denis
Malis, (si jina lake halisi) akiwa kwenye karakana yake kwenye eneo la Yambio jimboni Equatoria Magharibi nchini Sudan Kusini.

NchiniSudanKusini, watoto waliokuwa wametumikishwavitanina hatimaye kuachiliwa huru sasa wameanza kubadili maisha yao nayawengine baadayakupatiwa stadi za kujipatia kipato kwa msaada wa Umoja wa Mataifa na wadau wake.

NchiniSudanKusini, watoto waliokuwa wametumikishwavitanina hatimaye kuachiliwa huru sasa wameanza kubadili maisha yao nayawengine baadayakupatiwa stadi za kujipatia kipato kwa msaada wa Umoja wa Mataifa na wadau wake.

Miongoni mwa watoto hao ni Malis, si jina lake halisi ambaye sasa anamilikikarakanayakutengenzasamanihuko Yambiojimboni Equatoria Magharibi.

Malis ambaye sasa ana umri wa miaka 26 alitekwa nyara na kundi la watu wenye silaha akiwa bado barubaruna kupelekwa msituni ambapo anasema kuwa,“wakati tulipokuwa msituni, tulipata shida sana. Amani ilipopatikana nchini mwetu, tulitoka msituni na kujisalimisha na pia tulipatiwa mafunzo.”

Mapema mwaka 2018, Malis alibahatika kwani aliachiliwa huru na watesi wake kufuatia harakati zilizoongozwa na vikundi vya kidini na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchiniSudanKusini,.

Askofu Hiiboro Kusala wa kanisa katoliki DayosisiyaTombura na Yambio yeye ni mwenyekiti wa kikundi cha kidini na anazungumzia harakati za kuachiliwa kwa Malis na wenzake akisema kuwa,“tuliweza kukutana na watu hao msituni na kisha kuweza kuwatoa msituni zaidiyavijana 10,000 ambao walikuwa wanashikiliwa huko, vijana ambao walikuwa tayari kuua na hata kupigana. Na ni kwamba mara nyingi, jambo ambalo sipendi kusema, vijana hao walikuwa wanatufanya manyanyaso sana msituni lakini hatukukata tamaa.”

Kunasuliwa msituni, kumewezesha hii leo Malis awe na stadi za ufundi seremala akiwa na cheti baadayakumaliza mafunzoyamiezi 6yaufundi stadi yaliyofadhiliwa na UNMISS na wadau na kutekelezwa na shirika la World Vision katika chuo cha mafunzo stadi cha Tiindoka.

Malis anasema kuwa,“nilianza kujifunza jinsi wanavyopima vitu vyote mfano kukata na kuweka matundu.Nilijifunza vitu vyote hapo sasa naweza kutengeneza meza, viti na hata vitanda.Mtu anaweza kufika akapenda na tunazungumza na ananipatia fedha.”

Mafunzo yalimweza kuanzishakarakanayake na kutengenezasamanizinazohitajika kwenye jamii yake.

Malis si mchoyo wa ujuzi wake na hivyo katikakarakanayake anafundisha vijana wengine, miongoni mwao ni Isaac ambaye naye si jina lake halisi na anasema kuwa,“amenifundisha mambo mengi. Hivi sasa naweza kutengeneza vitu vingi kama vile vitanda, milango, kabati na vitu vingine vingi vidogo vidogo.”

UNMISS kwa upande wake inajivunia kwa kuwa kwa kufanya kazi na wananchi waSudanKusinikatika kujenga amaniyakudumu ndio jukumu lake.

Christopher Muchiri Murenga, ni mkuu wa ofisiyaUNMISS mjini Yambio na anasema kuwa,“tunataka kujenga mashauriano katiyajamii kuhusu kile walicho nacho na fursa za maendeleo kwenye jamii zao na changamoto wanazokabiliana nazo. Halikadhalika vitisho wanavyodhani wanawea kukumbana navyo na uthabiti na udhaifu wao ili hatimaye wao wenyewe wawe vichocheo vya kujenga mnepo na kusonga mbele katika kujikwamua na kuendelea.”

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto,, zaidiyawatoto 3,000 nchiniSudanKusiniwameachiliwa huru na vikundi vilivyojihami tangu kuanza kwa mapiganoyawenyewe kwa wenyewe nchiniSudanKusinimwezi Disemba mwaka 2013 na bado maelfu kadhaa wanatumikishwavitani.