Mialo ya ziwa Viktoria imejaa maji, mama lishe Mwanza wapaza sauti

Get monthly
e-newsletter

Mialo ya ziwa Viktoria imejaa maji, mama lishe Mwanza wapaza sauti

山News
15 May 2020
By: 
Wavuvi kutoka Kenya wakiwa katika harakati za uvuvi kwenye ziwa Victoria ambako Sangara ndiko makazi yake zaidi
FAO/Ami Vitale
Wavuvi kutoka Kenya wakiwa katika harakati za uvuvi kwenye ziwa Victoria ambako Sangara ndiko makazi yake zaidi

Ripoti za kuendelea kuongezeka kwa kina cha maji katika Ziwa Viktoria barani Afrika zimeendelea kuenea na sasa waathirika wa hali hiyo wanazungumza kupaza sauti zao ili waweze kupatiwa msaada wakati huu ambapo njia zao za kujipatia kipato zimeathiriwa na ongezeko la kiwango cha maji.

Rose ni miongoni mwa wakazi wa maeneo haya pembezoni mwa ziwa viktoria Mwanza Nchini Tanzania, Ziwa hili ambalo ni kubwa zaidi barani Afrika linatumiwa na Kenya, Uganda na Tanzania, likiwa ni makaazi, sehemu za biashara, kama mialo na sehemu za kupumzika na biashara ndogondogo. Hata hivyo kutokana mabadiliko ya tabianchi hali ni tofauti.

Kwa sasa ziwa hili limejaa maji kupita kiasi na kuathiri shughuli za kijamii na kiuchumi kandokando mwa ziwa hili kama anavyoeleza Rose akisema kuwa,"ndio hivyo maji yamekuwa mengi sana.Tumeathirika kwa kweli mpaka wengine wameamua kufunga vibanda kwa sababu ya maji. Tumepata madhara makubwa sana kwa sababu ya maji, maana uchafu unakuja wa kila aina tunashindwa tufanyeje, ila hatuna namna."

Pamoja na kukiri madhila ya ongezeko hilo Rose anaamini sababu kuu ya hali hii ni ongezeko la mvua tofauti na miaka iliyopita akisema ya kwamba, "ndio hivyo mwaka huu Mungu ameleta mvua nyingi. Mimi naamini ni mvua hakuna kitu kingine kwa sababu hata kwenye redio unasikia wanatangaza mikoa mingine inanyesha kuanzia asubuhi mpaka jioni. Ni mvua tu ndio imekuwa nyingi mwaka huu."

(Sauti ya Rose Venance)

Kwa upande wake Bernad Abel ambaye ni Msimamizi wa moja ya mialo anasema hali hii haikuwahi kushuhudiwa kwa hivi karibuni ....

(Sauti ya Bernad Abel)

Hata hivyo Bi Rose anaamini serikali inaweza kufanya jambo kupunguza athari hizi

(Sauti ya Rose Venance)