Mlipuko wa Ebola mashariki mwa DRC umetokomezwa, WHO yapongeza

Get monthly
e-newsletter

Mlipuko wa Ebola mashariki mwa DRC umetokomezwa, WHO yapongeza

山News
26 June 2020
By: 
Wauguzi wakisherekea mwisho wa janga la Ebola mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambapo wafanyakazi zaidi ya 200 walifanya kazi bila kuchoka kulinda watoto kutokana na ugonjwa huo.
UNICEF/Jean-Claude Wenga
Wauguzi wakisherekea mwisho wa janga la Ebola mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambapo wafanyakazi zaidi ya 200 walifanya kazi bila kuchoka kulinda watoto kutokana na ugonjwa huo.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,DRCimetangaza kutokomezwa kwamlipukowa10waEbolamasharikimwanchi hiyo ulioanza mwezi Agosti mwaka 2018.

Tangazo limetolewa hii leo kwenye mji mkuuwaDRC, Kinshasa na WaziriwaAfyawanchi hiyo,Dkt. Eteni Longondo, hatua ambayo imepongezwa na Mkurugenzi Mkuuwashirika la afya la UmojawaMataifa, , Dkt. Tedros Ghebreyesus.

Akizungumzia hatua hiyo, Dkt. Tedros amesema,“leo ni siku ya furaha, nafurahia kusherehekea kutokomezwa kwaEbolanchiniDRCambako zaidi ya watu 1,100 waliouguaEbolana kupona, walirejea na afya njema kwa familia zao na huu ni ushuhudawahuduma za tiba zilizotolewa na wafanyakaziwaafya nchini humo, wakiungwa mkono na WHO na wadau wengine.”

Ameongeza kuwa,“kutokomezwa kwaEbolani ushindiwasayansi. Kasi kubwa ya kupelekwachanjo yenye ufanisi mkubwakuliokoa maisha na kulipunguza kasi ya maambukizi na kwa mara ya kwanza sasa dunia ina chanjo iliyothibitishwa dhidi yaEbola. Tiba fanisi nazo zilibainishwa ambazo zilipunguza kwa kiasi kikubwa tishio pindi mgonjwa alipotibiwa haraka.“

Mkurugenzi Mkuu huyowaWHO ametuma pongezi za kipekee kwa madaktari, wahudumuwaafya na wafuatiliaji waliokwenda nyumba kwa nyumba kusaka wagonjwa wapya huku akikumbuka wahudumuwaafya waliopoteza maisha akisema WHO itaendelea kusisitiza umuhimuwausalama wao.

WHO imepongeza pia nchi 9 jirani naDRCambazo imesema zilikuwa na mchango mkubwa katika kutokomezwa kwaEbolaMasharikimwaDRC.

Hata hivyo WHO imesisitiza kuwa hakuna kubweteka kwa kuwa kunamlipukomwinginewaEbolahuko Mbandaka jimboni Equateur na kusema kuwa hata zilizochukuliwamasharikimwaDRCkutokomezaEbolazitumike pia Mbandaka na dhidi ya Surua na ugonjwawavirusi vya Corona au COVID-19.

Jumla ya watu 2,200 walifariki dunia kutokana namlipukohuowa10waEbolahukomasharikimwaDRCulioanza Agosti 2018.