Nilikuwa nakufa, wahudumu wameniokoa-aliyepona COVID-19

Get monthly
e-newsletter

Nilikuwa nakufa, wahudumu wameniokoa-aliyepona COVID-19

山News
28 April 2020
By: 
Adrien Bali, mwenye umri wa miaka 56 akizungumza katika hospitali ya Mtakatifu Joseph mjini Kinshasa, nchini DRC baada ya kupona COVID-19.
UNICEF VIDEO
Adrien Bali, mwenye umri wa miaka 56 akizungumza katika hospitali ya Mtakatifu Joseph mjini Kinshasa, nchini DRC baada ya kupona COVID-19.

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, mmoja wa manusura wa ugonjwa wa virusi vya Corona auamesihi raia wa taifa hilo la Maziwa Makuu Afrika waitikie wito wa kujikinga na gonjwa hilo akisema kuwa yeye ni shuhuda aliyenusurika.

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia yaCongo,DRC, mmoja wamanusurawa ugonjwa wa virusi vya Corona auCOVID-19amesihi raia wa taifa hilo la Maziwa Makuu Afrika waitikie wito wa kujikinga na gonjwa hilo akisema kuwa yeye ni shuhuda aliyenusurika.

Manusurahuyo Adrien Bali mwenye umri wa miaka 56 amesema haoy akizungumza kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto,, kwenye mji mkuu waDRC, Kinshasa.

Bwana Bali ambaye alipata huduma kwenye hospitali ya Mtakatifu Joseph jijini Kinshasa anasema kuwa,“nilikuwa mwenye afya njema lakini asubuhi ya jumapili kabla ya Pasaka, wakati nataka kunywa chai, nilikosa kabisa hamu ya kuinywa. Niliona chakula kama tope na sikuweza kumeza kitu chochote. Siku ya jumatatu, nilianza kukosa pumzi na jioni ilipofika sikuweza kupumua kabisa.”

Bali ambaye anatoka wilaya ya Limete jijini Kinshasa ameendeleza simulizi yake akisema kuwa,Jumanne nilikuwa nakufa, nilishindwa kupumua. Nilimpigia simu daktarin wangu ambaye ilibidi azungumze na mke wangu kwa sababu sikuweza kuendelea kuzungumza naye. Lakini nilinikuwa nakufa. Ilikuwa ni virusi vya Corona, sikuweza kupumua. Kama wasingaliniwekea mashine ya kunisaidia kupumua nilikuwa nakufa. Kwa hiyo huduma katika hospitali ya Mtakatifu Joseph ni nzuri sana.”

Kupona kwa Bwana Bali, kumempatia fursa ya kupaza sauti kwa raia waDRCakiwaambia kuwa,Natoa wito kwa wakongo wenzangu, kwa sababu nimanusura, tafadhali tambuein umuhimu wa kuvaa barakoa na kutochangamana, muwe umbali unaotakiwa ili tuondokane na janga hili.”

Kwa mujibu wa takwimu za shirika la afya la Umoja wa Mataifa,,DRCina jumla ya wagonjwa 459 ambapo kati yao hao28 wamefariki dunia.