UNHCR yagawa msaada kwa waomba hifadhi Libya kwa ajili ya COVID-19 na Ramadhan

Get monthly
e-newsletter

UNHCR yagawa msaada kwa waomba hifadhi Libya kwa ajili ya COVID-19 na Ramadhan

山News
20 May 2020
By: 
Mwanamke raia wa Somalia akiwa na mtoto wake wa umri wa mwaka mmoja katika kituo cha Ganfoda karibu na Benghazi baada ya kuyakimbia machafuko katika nchi yake na kuingia kinyume cha sheria Libya.
UNICEF/Giovanni Diffidenti
Mwanamke raia wa Somalia akiwa na mtoto wake wa umri wa mwaka mmoja katika kituo cha Ganfoda karibu na Benghazi baada ya kuyakimbia machafuko katika nchi yake na kuingia kinyume cha sheria Libya.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limegawa msaada wa dharura kwa mamia ya wakimbizi, wahamiaji na waomba hifadhi mjini TripoliLibya, wakati huu hali ikizidi kuzorota kutokana na machafuko, vikwazo vya kupambana na janga la corona auCOVID-19.

Kwenye makazi ya waomba hifadhi mjini Tripoli lori nalimesheheni msaada linaouga kwa wakimbizi, wahamiaji na waomba hifadhi ambao unajumuisha chakula cha mwezi mzima, vifaa vya kujisafi na tembe za kusafisha maji zinazotolewa na shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa.

Maelfu ya wahamiaji na waomba hifadhi wanahaha hivi sasa nchini Libya kuweza kuishi sababu kazi hakuna kutokana na hatua za kupambana na janga la corona au COVID-19 na makazi yao yaliyofurika yanafanya hatua ya kujitenga kuwa kama ni starehe.

Ramani ya kusambaa kwa COVID-19 duniani

Na hali imekuwa mbaya zaidi kwa wanaofunga mwezi mtukufu wa Ramadhan hivyo UNHCR imeamua kuchukua hatua kuwasaidia. Zeinab Farhat ni afisa msaidizi a masuala ya ulinzi wa shirika la UNHCR,“Ramadhan ni wakati muhimu wa kuonyesha mshikamano na msaada kwa watu wenye mahitaji, hasa wakati huu vita vikishika kasi na amri za kutotembea zikiwekwa kuzuia kusambaa kwa COVID-19, na kufanya kuwa vigumu kwa watu kupata ajira ya kuendesha maisha yao. Huu ni mgao wa kwanza wa dharura tunaufanya kwa mwezi huu na tunatarajia kuwafikia wakimbizi na waomba hifadhi 4000 kwa msaada ikiwemo chakula.”

Wakati nchi nyingine hivi sasa zikiongeza juhudi za kupambana na corona Libya inasalia kughubikwa na vita ambavyo havijapungua licha ya hatua za kusalia majumbani kujikinga na corona.

Na janga hilo limeongeza adha kwa wahamiaji na waomba hifadhi hawa huku wengine wakishindwa hata kulipia gharama za pango na mahitaji ya lazima , miongoni mwao ni Robel mkimbizi kutoka Eritrea,“nilikuwa nafanyakazi kama kibarua wa siku, lakini sasa ni vigumu kwa sababu ya corona. Nimeshindwa kupata kazi kwa mwezi mzima uliopita. Tuna wagonjwa na hatuwezi kulipa kodi ya pango na kama una simu na unatembea mitaani ni tishio”

Msaada huu uliogawanywa na UNHCR umekusanywa kwa ushirikiano na serikali na wadau wengine wa misaada, shirika la LibAid na kamati ya kimataifa ya uokozi IRC.