Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR leo limetoa omboi la dola milioni 186 kwa ajili ya kutoa msaada wa kuokoa Maisha na ulinzi kwa wakimbizi, wakimbizi wa ndani, watu wanaorejea makwao na jamii zinazohifadhi wakimbizi katikati mwa ukanda wa Sahel.
Ombi hilo linajumuisha dol milioni 97 za mahitaji ya mwazo kwa mwaka huu wa 2020, dola zingine milioni 29 kwa ajili ya utekelezaji wa mipango ya kupambana na janga la corona au COVID-19 kwenye maeneo waliotawanywa wat una dola zingine milioni 60 za kuongeza hatua za dharura za kama sehemu ya mkakati wake Sahel.
Akizindua ombi hilo mjini Geneva Uswis kamishina mkuu wa wakimbizi Filippo Grandi ameelezea ukarimu mkubwa wa jamii zinazohifadhi wakimbizi katika ukanda huo , lakini pia ameweka wazi kwamba zimezidia hadi pomoni hususan Burkina Faso ambako idadi ya wakimbizi wa ndani imeongezeka Zaidi ya mara nne kutoka 193,000 Juni mwaka 2019 na kufikia 848,000 mwishoni mwa mwezi Aprili mwaka huu.鈥滵harura ya Sahel ni mgogoro wa kibinadamu na wa ulinzi wa kiwango kikubwa sana, ambako machafuko dhidi ya watu wasion a hatia yamegeuka janga. Hatari ya kusambaa zaidi machafuko hayo katika nchi jirani iko bayana na sasa janga la COVID-19 limefanya hali kuwa mbaya zaidi.鈥
Kwa watu ambao walikimbia vita na mauaji na kwa jamii ambazo zimewapokea kwa ukarimu mkubwa, athati za COVID-19 kwa uwezo wao wa mlo wa siku tu imekuwa vigumu sana kuendelea kuishi. Grandi ameongeza kuwa 鈥淭unahitaji kuongeza msaada wetu kwa mipango ya kina na jumuishi ambayo inauweka ustawi na haki za mamilioni ya wakimbizi wa ndani katika kitovu cha tunayofanya. Lazima tuchukue hatua sasa kabla hatujachelewa.鈥
Kupitia ombi hili UNHCR itaweza kutoa msaada wa malazi Zaidi ili kupunguza msongamano katika maeneo yaliyofurika, msaada wa vifaa muhimu听听na kukabiliana na ukatili wa kijinsia na kingono ambo umesambaa san ana kukita mizizi katika maeneo yaliyofurika.
Pia itamaanisha kwamba UNHCR itaweza kusaidia masuala ya elimu, ujenzi mpya wa shule na madarasa au kutoa fursa za Watoto kusoma wakiwa mbali.
Kuna jumla ya watu milioni 3.1 ambao ni wakimbizi, wakimbizi wa ndani, wanaorejea na walio katika hatari ya kutokuwa na utaifa kwenye ukanda wa Sahel. Serikali za Burkina Faso, Chad, Mali, Niger na Mauritania ziliahidi kutoa ulinzi na suluhu kwa makundi haya zilipotia Saini azimio la Bamako mwaka 2019.