缅北禁地

UNMISS waendesha warsha kwa wanawake ya kutoa mafunzo ya kutatua mizozo

Get monthly
e-newsletter

UNMISS waendesha warsha kwa wanawake ya kutoa mafunzo ya kutatua mizozo

缅北禁地News
6 March 2020
Wanawake wakizungumza kwenye kampeni ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake, Sudan Kusini. Kushoto ni Dudu Emilia.
UNMISS/Nektarios Markogiannis
Wanawake wakizungumza kwenye kampeni ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake, Sudan Kusini. Kushoto ni Dudu Emilia.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS, kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali听la kupinga ukatili kwa ajili ya amani wameaanda warsha ya wawakilishi wanawake takriban themanini kuhusu namna ya kuzuia mizozo na kulinda haki za binadamu.

Katika kambi ya Rimenza inayozingira kanisa la Equatoria听magharibi nchini Sudan Kusini shughuli za kila siku zinaendelea lakini kwa upande mwingine, washiriki wa warsha wanabadilishana uzoefu wao kuhusu mbinu za kutatua mizozo kwa lengo la kuwa mabalozi wa amani katika jamii yao.

Washiriki wanafanya zoezi kwa vitendo ni katika kuelimishwa kuhusu kutatua mizozo kwa njia ya amani听

Mmoja wa washiriki ni Mama Tubi Festus mkazi wa kambi ya wakimbizi wa ndani ya Rimenze,鈥淭umejifunza mengi kuhusu mizozo, jinsi ya kukabiliana nayo na ni nini athari zitokanazo na mzozo ambao听zinaathiri听jamii yetu.鈥

Washiriki hao wamepata wataalamu ambao wamewaelimisha kuhusu mizozo na hivyo wana matumaini katika kukabiliana na hilo kama anavyoafiki Mary Papai Wangu, mkazi wa kambi ya Rimenze,鈥淜ile ambacho nitafanya baada ya mafunzo haya ni kwamba, watu ambao nitakutana nao wanaokabiliwa na mzozo, nitajaribu kusuluhisha kwa kutumia stadi ambazo nimezipata katika warsha hii ya siku mbili.鈥

听inaamini kwamba ni muhimu kuimarisha wanawake kwa ajili ya kuhimiza uwiano katika jamii kama anavyosema Jackson Kambale, afisa wa maswala ya umma听wa mpango huo

鈥淭uliwaza na kukubaliana na wanawake katika eneo hili kwamba wanahitaji stadi muhimu na mbinu za kuwasaidia kuchangia katika utengamano katika eneo hili na kujenga mahusiano thabiti miongoni mwao kwa ajili ya kukabiliana na mizozo ambayo huenda ikaibuka hapa.鈥

Na baada ya kukamilisha warsha, nyimbo na vigelegele vikatamalaki.