Idadi ya wagonjwa wa virusi vya Corona, au COVID-19 nchini Kenya ikifikia 3000, serikali hii leo imetangaza mkakati wa kuepusha vituo vya afya na hospitali kuzidiwa uwezo wa kutibu wagonjwa hao.
Msemaji wa serikali ya Kenya Cyrus Oguna akizungumza jijini Nairobi, Kenya, amesema kuwa wagonjwa waliothibitishwa kuwa na virusi watatibiwa hospitalini, lakini wale wasio na dalili zozote za ugonjwa wataugulia makwao.
Itawezekana tu kwa sababu ni kitu ambacho kinafanyika na nchi zingine. Ni kitu cha kawaida tu na ni kitu ambacho kwetu kwa sababu ya mazingira tunamoishi. Mtu听 akibainika kuwa na virusi wanamwangalia na kama hana dalili zozote watafanya uchunguzi kuangalia sehemu anamoishi ni sehemu ya aina gani. Kama ana pahali听ambako yeye mwenyewe anaweza kujihifadhi na kujitenga na watu wengine wa nyumbani, basi atapelekwa nyumbani na apewe wahudumu wa afya wanaojitolea katika jamii, ili waweze kumchunguza. Lakini pia kutakuwa na mawasiliano na yeye iwapo ameona dalili zozote. Kutakuwa na mawasiliano ya karibu听 baina yake na听wafanyakazi wa afya ya jamii wakujitolea.
Idadi ya wagonjwa wa COVID-19 imeongezeka kwa kasi tangu mgonjwa wa kwanza aripotiwe mwezi Machine mwaka huu na idadi ya wagonjwa inatarajiwa kuongezeka kutokana na kuendelea kwa upimaji wa virusi hivyo.
Akizungumzia hatua ya leo ya serikali, Dkt. Ahmed Khalebi kutoka maabara ya Lancet anasema kuwa hatua ya kuwatibia wagonjwa majumbani ingeanza kitambo
Sijui kwanini hapa nchini kwetu na sehemu zingine za Afrika watu walijaribu kuweka watu ambao wana virusi vya Corona kwenye hospitali na mtu hana dalili. Ukienda nchini zote Ulaya, Amerika watu hawapelekwi hospitalini hadi pale wanapozidiwa. Kwa hivyo hakuna haja ya mtu kupelekwa hospitalini ama kwenda kupelekwa kwenye karatini kama anaweza kukaa nyumbani kwake. Kuliko kwenda kwenye karantini mahali ambapo kwa mfano watu wanatumia sehemu za kujisafi kama vyoo kwa pamoja ,faida gani kwenda kuweka mtu na watu wengine wa nje ambao ikiwa kuna Corona atakuwa ashapata? kwa hivyo hili ni jambo tumezungumza kwa muda mrefu zaidi ya miezi miwili lakini kwa sasa naona imezungumza na kutia mkazo na serikali pia.