Ni saa tatu asubuhi jua limeshaanza kutoa miale yake katika makazi ya wakimbiziya Bidibidi katika Wilaya ya Yumbe nchini Uganda. Wanawake wamekusanyikakaribu na kisima cha maji ili kuchota maji ya asubuhi halafu watarudi tena papa hapa jioni.
Joyce Maka mwenye umri wa miaka arobaini anasubiri wanawake zaidi wafikekatika eneo la kuchota maji. Yeye ni mkimbizi mama wa watoto watatu alifikakutoka Sudani Kusini mnamo 2018, baada ya waasi kumuua mumewe. Leo, yeye ni miongoni mwa wapatanishi wa amani 12 wanawake katika Kanda ya pili ya makazi ya Bidibidi, na yuko hapa kuwahamasisha wenzake kuhusu听 hatua za kujikinga na COVID-19 - ugonjwa ambao umesababisha kuzorota kwa maisha ya watu na uchumi ulimwenguni. Watu wanaoishi katika makazi ya wakimbizi wako katika hatari kubwa zaidi ya
gonjwa hili, kwa kuwa wanaishi katika makazi yasiyo rasmi na bila huduma za msingi na mifumo ya afya inaweza kuzidiwa haraka sana. Hatua zilizotangazwa kama vile kukaa nyumbani ili kuzuia kuenea kwa COVID-19 zimeleta changamoto
katika kuhakikisha kila mtu anapata habari za jinsi ya kujikinga.
Maka anasema maeneo ya uchotaji wa maji bado huwavutia watu na kawaida wanawake na wasichana kwa idadi kubwa na kwa hivyo hizi ni sehemu za kimkakati za kupitisha ujumbe wa habari za kuokoa maisha. Tunawahimiza kukaa angalau mita mbili kutoka kwa kila mmoja; tunawahimiza pia wanawe mikono yao kabla na baada ya kuchota maji. Wakati idadi ya kesi za COVID-19 nchini Uganda zinaendelea kuongezeka, wanawake wapatanishi wa amani wanaosuluhisha mizozo na changamoto za jamii, wamejiunga na mapigano hayo katika makazi ya wakimbizi wilaya za Yumbe na Adjumani, zinazopakana na Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Kufikia 9 Juni, Uganda imerekodi maambukizi 646.
Mradi wa Umoja wa Mataifa wa Wanawake, kwa kushirikiana na Kituo cha Amani cha Wanawake cha Kimataifa, na kufadhiliwa na Serikali ya Norway, umetoa mafunzo na kuunga mkono wapatanishi wa amani wa wanawake 160 katika wilaya za Yumbe, Adjumani na Kotido. Wakati kazi yao kawaida inajumuisha kuleta amani na suluhisho kwa mizozo ya jamii, pamoja na vurugu za nyumbani, ndoa za mapema na masuala ya haki za ardhi, mradi huo uliwekwa ili kusaidia kuelimisha jamii kuhusu听 hatua za kuzuia za COVID-19. Wamejifunza juu ya umuhimu wa kunawa mikono, kutochangamana, kuvaa barakoa na kutoa taarifa kwa wahamiaji wapya ili waweze kupimwa na kuwekewa kwenye karantini. Wanawake wa Umoja waMataifa听pia wametoa barakoa, sabuni na vifaa vya wakati wa hedhi kwa usalama wao.
Mtaalam wa Usimamizi wa Programu ya wanawake ya Umoja wa Mataifa, Yusrah Naguuya anasema kuwa ;tulitaka kuhakikisha kuwa wapatanishi wa amani wa wanawake wamelindwa dhidi ya COVID-19. Tunawahimiza wachukue
tahadhari muhimu, wasiweke maisha yao, familia na jamii kwa ujumla katika hatari.
Katika makazi ya Nyumazi wilayani Adjumani, wapatanishi wanalenga sehemu za usambazaji wa chakula kupitisha ujumbe kuhusu COVID-19. Pia wanakutana na watu barabarani ili kuwa na mazungumzo ya moja kwa moja, kuhakikisha kwamba kila kaya inalo eneo la kuosha mikono, mahali safi pa kuhifadhi vyombo na upatikanaji wa vyoo.
Martha Achok, mpatanishi wa amani kutoka Nyumazi anafafanua kwamba kazi ya kuzuia COVID-19 inaweza kuwa ngumu sana katika makazi ya wakimbizi:Ni jambo linaloonekana kama mzaha kumwambia mtu anawe mikono yake kwa kutumia sabuni mara mingi wakati anakaa kwa muda wa wiki bila kufua nguo zake kwa sababu ya ukosefu wa sabuni. Bado tunawashauri kwa sababu kunawa mikono pia ni suala la kitabia. Hata wakati kuna sabuni mtu anahitaji kukuza tabia ya kunawa mikono mara kwa mara.鈥滺uku听 Bidibidi, wapatanishi wametunga nyimbo katika lugha yao ili kupitisha ujumbe kwa urahisi hii ni njia ya mawasiliano ambayo ni mwafaka kabisa kwa wakazi. Achok tayari ameona mafanikio kadhaa katika kuongeza mwamko. Maambukizimengi ya sasa ya COVID-19 katika makazi hayo zinajumuisha wahamiaji wapya. Jamii sasa zimekuwa makini zaidi katika kutambua wageni ili kuhakikisha kuwa wanapimwa na kuweka kwenye karantini kwanza, ambayo imesaidia kudhibiti
kuenea zaidi kwa ugonjwa huo.Mary Aemo, afisa wa jamii wa Kituo cha Amani cha Wanawake cha wilayani Yumbe anasisitiza kwamba kupata uaminifu na ushirikiano katika jamii ni ufunguo wa kuzuia kufanikiwa kwa kuenea kwa COVID-19, na wapatanishi ni wanachama wanaoaminika wa jamii,idadi kubwa ya watu inachukua mambo haya kwa uelewa kwa vile wanaripoti jamaa ambao wanakuja kutoka Sudan Kusini. Mmoja wa wapatanishi wa amani aliripoti mumewe mwenyewe ambaye alikuwa amerudi kutoka Sudan Kusini. Alipimwa na kuwekwa kwenye karantini na matokeo yalikuwa sawa.
Programu ya Shirika la Umoja wa Mataifa ya Wanawake nchini Uganda inatoa mifano ya jinsi ya kutumia azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa namba 1325, ambalo linahitaji ushiriki wa maana wa wanawake na uongozi katika ujenzi wa amani, maendeleo na mipangilio ya kibinadamu. Mwisho wa siku, kwa amani endelevu na utatuzi mzuri wa matatizo haitoshi kuhudumia mahitaji yawanawake pekee, ni muhimu pia kuwashirikisha kama viongozi katika kuchagiza
vitendo na maamuzi katika jamii zao.