Wasichana wasiogope sayansi kwa sababu inatuzingira kila mahali- Bi Wahome
Get monthly
e-newsletter
Wasichana wasiogope sayansi kwa sababu inatuzingira kila mahali- Bi Wahome
Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake na wasichana katika sayansi, Shirika la Umoja wa mataifa linalohusika na masuala ya wanawake, UN- Women na lile la听 elimu sayansi na utamaduni, UNESCO yamesema sauti za wanawake na wasichana na ujuzi katika sayansi, teknolojia na ubunifu ni muhimu katika kuleta suluhu katika Dunia ya sasa ambayo inashuhudia mabadiliko ikiwemo mabadiliko haribifu.
Halikadhalika mashirika hayo yamesema kuna haja ya kuziba pengo katika sekta ya sayansi, teknolojia, uhandisi na hisibati, STEM na kuimarisha usawa wa kijinsia katika kazi husika.
Kauli hiyo imethibitishwa na Anastasia Wahome,听mkuu wa kitengo cha sayansi na takwimu听听katika shirika la kikanda la kiserikali linalousika na usimamizi wa rasilimali kwa ajili ya maendeleo lililoko jijini Nairobi, Kenya听 akisema kuwa听bado wasichana hawajakumbatia masomo ya STEM kama inavyohitajika kwa kuwa wasichana wengi bado wana hofu ya kujifunza masomo hayo kutokana na kukosa watu wa mfano kwao.
Akaenda mbali zaidi na kutoa wito kwa听wasichana ambao wangependa kujikitia katika masomo ya sayansi wajitokeze.