Viwavi wanaochagiza warejea katikakati ya janga la COVID-19

Get monthly
e-newsletter

Viwavi wanaochagiza warejea katikakati ya janga la COVID-19

Afrika Mashariki yavamiwa na wimbi la pili la nzige na kuwacha mamilioni katika hatari ya kukosa chakula
28 May 2020
 Desert Locust Swarms
Sven Torfinn, FAO
Wingu la nzige

Huku visa vya COVID-19 vikiendelea kuongezeka kote Afrika, Afrika Mashariki inakabiliwa na hatari nyingine. Wimbi la pili la nzige wa jangwani linatishia kuharibu mimea mipya miezi michache tu baada ya mawingu ya kwanza ya nzige kulishambulia eneo hili, ambako zaidi ya watu milioni 20 wanakabiliwa na tishio la uhaba wa chakula.

"Hili limetukia wakati mbaya sana, kwa kuwa ndipo wakulima wanapanda sasa, na miche imeanza kuchipuka sasa kwa kuwa ni mwanzoni mwa msimu wa mvua,” asema Keith Cressman, Afisa Mkuu Mtabiri wa Nzige wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO).

Msimu wa mvua wa mwezi wa Februari hadi Mei ndio wakati murua wa wakulima kupanda mimea, huku uvunaji ukitarajiwa kuanzia Juni hadi mapema Julai, ambao ndio wakati hasa wingu jingine la nzige linatarajiwa. Mvua imenyesha vyema mwaka huu, na mazingira ya unyevunyevu ni mwafaka kabisa kwa mayai ya nzige kuanguliwa.

Nzige wa jangwani wanatambuliwa kama wadudu waharibifu zaidi wa kuhamahama duniani. mkurupuko wa sasa ulianza kwa sababu ya mvua kubwa kufuatia tufani mbili mwezi wa Mei na Oktoba 2018 katika rasi kusini mwa Arabia. Kufikia sasa nzige hawa wameenea kupitia Djibouti, Uhabeshi, Eritrea, Kenya, Tanzania, Uganda, Somalia, Sudan Kusini, Yemen, na kote katika Ghuba la Uajemi.

Wingu moja linaloenea kilomita moja mraba lina hadi jumla ya nzige milioni 80. FAO linakadiria huenda idadi ya nzige ikaongezeka mara 20 msimu huu wa mvua na kuzidisha hatari ya kibinadamu.

Kudhibiti suafiri kwa sababu ya COVID-19 kumefanya shughuli ya kukabili nzige kuwa hata ngumu zaidi. FAO linaongeza msaada kwa nchi zilizoathiriwa licha ya changamoto za taratibu za usafiri, likishirikiana na serikali za kitaifa, wakulima na wazalishi wa kilimo kusaidia kudhibiti hali hii.

"Hakuna kusitisha kasi hasa kwa kuwa nchi zote zilizoathirika zinawapa nzige wa jangwani kipaumbele kwa masualaa ya kitaifa,” alisema Cyril Ferrand, Nahodha wa Kikosi cha Resilence cha Afrika Masharika cha FAO. Aliongeza, “Huku sheria ya kusalia

nyumbani ikichukua uhalisi, watu wanaokabiliana na ongezeko la nzige wanakubaliwa kushika doria na kufanya makabiliano ardhini na hewani.”

FAO linazidisha shughuli ya kuchukua data kupitia kwa mtandao wa washirika, asasi za kiraia, maafisa wa nyanjani na mashirika ya mashinani wakitoa habari kutoka maeneo ya mashambani hasa nchini Uhabeshi, Kenya, Somalia na Sudan Kusini.

Shirika hilo pia linatoa msaada katika juhudi za ushikaji doria pamoja na unyunyiziaji dawa ardhini na hewani katika mataifa 10. Zaidi ya ekari 240,000 zimetibiwa kwa dawa za wadudu za kemikali na zile zinazoundwa kutokana na viumbe uhai katika eneo hilo na watu 740 wamepewa mafunzo kukabiliana na nzige ardhini. Lakini janga la COVID-19 limeharibu ugavi wa vifaa vya kunyunyizia na dawa za wadudu kwa magari.

Njia bora zaidi ya kutibu mashambulizi ya mawingu ya nzige kwa sasa ni kunyunyizia kutoka hewani dawa zilizoundwa kutokana na viumbe hai kwa kutumia ndege. Vifaa vya kunyunyizia vinaagizwa kutoka mataifa kama Morocco, Uholanzi au Japan. Hata hivyo, kwa sababu ya kanuni ya kusalia nyumbani, mikondo ya kimataifa ya ugavi imeporomoka, ucheleweshaji na bei kuongezeka, na hali ya kutegemeka kushuka mno.

"Changamoto kuu tunayoikabili kwa sasa ni ugavi wa dawa za wadudu na kuna ucheleweshaji kwa kuwa usafiri wa ndege kimataifa umepungua pakubwa,” alisema Bwana Ferrand.

Aliongeza: "Tunalowekea kipaumbele hasa ni kuhakikisha kwamba dawa za wadudu haziishi katika mataifa hayo. Hilo litakuwa tishio kwa watu wa mashambani au riziki zao na utoshelevu wao wa chakula unategemea ufanisi wa kampeni yetu ya kudhibiti hali.