Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC) Bw. Moussa Faki Mahamat alianzisha hazina ya Kuwajibikia COVID-19 ya Umoja wa Afrika (AU) ili kuimarisha uwajibikiaji wa janga hili wa bara Afrika mwezi Machi 2020. Baada ya kuchangisha dola milioni 44 kufikia Oktoba 2020, juhudi nyingine ya kuchangisha dola milioni 300 zaidi ilizinduliwa mwezi huo. Katika mahojiano na Kingsley Ighobor wa Afrika Upya, ProfesaÌýBenedict OramahÌýanaeleza jinsi Afrika inavyokusanya fedha na ni kwa nini michango zaidi inahitajika kwa dharura. Ìý
Kama Mwenyekiti wa Bodi ya WafadhiliÌý(Board of Trustees)Ìýwa Hazina ya Kuwajibikia COVID-19 ya AU, ni mambo yapi matatu uliyofaulu kutimiza kufikia sasa na ni changamoto zipi ulizokabiliana nazo? Ìý
Hazina ya Kuwajibikia COVID-19 ya AU (AU COVID-19 Response Fund)Ìýilibuniwa na Umoja wa Afrika kama Wajibikio la dharura kwa janga hili. Iliundwa kimsingi ili kulifanya bara hili kuwa na mwelekeo wa Afrika yote dhidi ya janga hili. Tuna chumi 55 zilizotengana. Na ukikumbuka Aprili mwaka jana, mambo makuu yalikuwa vifaa vya kujilinda binfsi (PPE) na vifaa vya kupima, na mataifa ya chumi kuu yalikuwa yakivinunua vyote vilivyokuwemo. Watengenezajiji hawakutaka kuyasikiliza mataifa madogo kiuchumi yakiagiza vifaa vya thamani ya elfu au milioni chache za dola. Kwa hivyo, hazina ya kuwajibikia ulikusudia kutusaidia kukabiliana na masuala kama hayo.Ìý Ìý
Pindi bodi ilipoundwa, tuliweka miundomsingi iliyohitajika kutuwezesha kufanya kazi kwa njia fanifu. Tulitakiwa kusaidia katika mambo mawili: kukusanya fedha na kusaidia katika matumizi ya fedha hizo. Kwa hivyo tuliunda kamati ndogo mbili muhimu kwa kasi kuyatimiza haya. Bila shaka, kimsingi tunatumikia Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Maradhi vya Afrika (CDC).Ìý
Tuliizindua shughuli ya kukusanya fedha mapema vya kutosha kwa usaidizi wa Umoja wa Afrika, wakati huo chini ya uwenyekiti wa Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, na kwa msaada wa Mwenyekiti wa Kamisheni ya AU BwanaÌý ÌýMoussa Faki Mahamat; Mkurugenzi wa Kituo cha Kudhibiti Maradhi cha Afrika ÌýDkt. John Nkengasong; Kamishna wa Masuala ya Kijamii wa AU Bi. Amira ElFadil miongoni mwa wengine. Tunajaribu kuhakikisha ahadi zote zilizotolewa za fedha zinatimizwa. Fedha hizi zinatoka haswa kutoka kwa mataifa ya Umoja wa Afrika, na kwa washirika wa kimaendeleo wa AU—Serikali ya Ujerumani, Serikali ya Uingereza na wengine.
Je, mna fedha za kutosha tunapozungumza sasa?Ìý
Hatuna fedha za kutosha kwa kuwa tunazitumia pindi tunapozipokea. Kuhusu suala la kuzikusanya, ninaamini kwamba tuna ahadi nzuri za fedha ambazo tunastahili kupokea. Tulipanga shughuli ya uchangishaji ambapo sekta ya kibinafsi ilishiriki. Na wengi wao wametoa ahadi. Tunachokifanya sasa ni kuhakikisha kwamba tunazigeuza ahadi hizo kuwa fedha—ahadi kutoka kwa serikali, kutoka kwa washirika wa kimaendeleo, kutoka kwa sekta ya kibinafsi.
Tunataka kuchangisha fedha, na kwa madhumuni hayo, hivi maajuzi tulimwajiri mshauri wa kukusanya fedha ambaye atatusaidia kukusanya fedha na kuhakikisha kwamba ahadi zilizotolewa zimegeuzwa kuwa fedha.
Je, tuna fedha za kutosha? La, mahitaji ni mengi kwa kuwa tunawafadhili wawajibikiaji wa upesi. Tunayafadhili mataifa yanayohitaji kupata vifaa vya matibabu. Hata sasa tunakisaidia Kituo cha Kudhibiti Maradhi cha Afrika na utekelezwaji wa shughuli ya kutoa chanjo. Kwa hivyo, tunahitaji fedha ili kuifanya kazi inayohitajika kufanywa. Hiyo ndiyo sababu tunafanya mpango wa uchangishaji fedha uliotiwa nguvu mpya ili kuhakikisha kwamba tunajaliza fedha ambazo tayari zinakusanywa, ikiwa ni pamoja na kupitia kwa Kituo cha Kudhibiti Maradhi cha Afrika. Aidha tunahimiza kwamba wanaweza kuchangia kupitia kwa Kituo cha Kudhibiti Maradhi cha Afrika. Tukizijumuisha fedha zote kufikia sasa, mbali na zile zinazokusanywa kando na Kituo cha Kudhibiti Maradhi cha Afrika tunazungumzia ahadi za zaidi ya $ milioni 100.Ìý
Ni changamoto ilioje kuwafanya wafadhili kutimiza ahadi zao za kifedha?
Vizuri, mambo ni magumu siku hizi. Kampuni zinapambana siku hizi; mataifa yanapambana. Kwa kiasi hicho, ndio, utimizwaji wa ahadi za kifedha zilizotolewa unafanyika polepole kuliko tulivyotarajia.Ìý
Hata hivyo, ni sharti niyapongeze mataifa mengi ya Afrika ambayo, licha ya changamoto hizo, yamejitokeza sio tu kutoa ahadi hizo bali kulipa. Manufaa ya kulipa ni kwamba kunarahisha msukumo wa kuingilia kati kwetu kwa manufaa ya Afrika yote. Ninatoa mfano: tulitoa msaada ili kununua dawa aina ya dexamethasone, moja kati ya dawa zinazotumiwa kutibu COVID-19. Sehemu moja ya ufadhili ulitoka kwa Wakfu wa Bill and Melinda Gates nasi tukatoa ufadhili sawia na huo.Ìý
Hebu tuizungumzie mipango. Iwapo hatuwezi kuishughulikia mipango ya ugavi, mataifa ambayo ni visiwa yatalipa zaidi ya mengine. Kwa hivyo, tunapoufanya ununuzi, tunafanya ugavi sawa na wa haki wa baadhi ya bidhaa hizi ili mataifa husika yazipate kwa karibu wakati sawa na bila gharama ya ziada. Hii ndiyo sababu tunayasihi mataifa ya Afrika ambayo hayajatoa ahadi kuzitoa ahadi hizo na yale ambayo yametoa ahadi lakini hayajazitimiza yatimize ahadi hizo, huku tukiwasihi wafadhili, ikiwa ni pamoja na biashara za Kiafrika, kutoa michango yao.ÌýÌýÌý Ìý
Baadhi ya michango iliyopokelewa kuhusiana na chanjo ni pamoja na ule uliotolewa na MTN [Kampuni moja ya mawasiliano ya rununu]. Mchango huo unatengwa na ile inayokuja kupitia kwa AVATT [Jopokazi la Kupokea Chanjo za Afrika yaani, Africa Vaccine Acquisition Task Team]. MTN iliahidi takriban dola milioni 25, ambazo tumetumia katika ugavi wa chanjo.
Je, mnawezaje kushirikiana kwa ufanisi na Kituo cha Kudhibiti Maradhi cha Afrika na Taasisi nyingine za mwelekeo wa Kiafrika zinazohusika katika uwajibikiaji huu?
Hazina hii [AU COVID-19 Response Fund] imeundwa na AU. Tulikuwa tukikutana kila wiki ila sasa tunakutana mara moja kwa mwezi. Washiriki wa mikutano hiyo ni pamoja na Kituo cha Kudhibiti Maradhi cha Afrika, na wanachama wa Bodi ya Wadhamini wanotoka katika pembe zote za Afrika—kaskazini, mashariki, magharibi na kusini. Tuna washiriki kutoka katika sekta ya kibinafsi. Tunayafikia mataifa kupitia kwa utaratibu huu. Tunapohitajika kuvishughulikia vitu ambavyo ni mahususi kwa kanda fulani, wanachama wa bodi ya wadhamini kutoka katika kanda hiyo watachukua jukumu kuhusu hiloÌý
Je, Afreximbank imechangia mfuko huo?
Bila shaka, Afreximbank imekuwa ikitoa msaada, sio tu kwa kuwa ninatoka katika Afreximbank, lakini pia kwa imani ya shughuli za benki hii. Tulitoa ahadi ya mchango ambayo tulilipa. Aidha, tunatoa ufadhili mwingine ambao si mchango wa fedha haswa kama vile raslimali watu. Kama nilivyosema, tulimwajiri na tumamlipa mshauri wa kukusanya fedha mshahara.
Je, ni usaidizi upi unaotolewa kwa mataifa na Afreximbank kukabiliana na janga hili?Ìý
Vizuri, wacha nianze kwa kusema kwamba tunafahamu vyema kukabiliana na matatizo kwa kuwa sisi ni benki iliyoundwa kutokana na matatizo. Afreximbank iliwaziwa miaka ya 1980 tulipokuwa na tatizo la deni. Tangu tuanze shughuli mwaka 1994 kumekuwa na matatizo mengi na benki ikachukua hatua. Ni kana kwamba tuna zana za kuyachukulia hatua matatizo.
Hiyo ndiyo sababu hata mapema kama Machi 2020, tulizindua Mfuko wa Kupunguza Athari za Janga Tandavu kwa Biashara, ambao uliundwa kuyasaidia mataifa kujirakibisha kwa tatizo hilo, kwa njia utaratibu. Kwa kutumia mfuko huo, kufikia sasa tumetoa dola bilioni 7, na fedha hizo ziliyasaidia mataifa mengi kulipa madeni ya kibiashara yaliyohitajika kulipwa. Tulifahamu kwamba iwapo hatungeyasaidia mataifa na yakose kulipa madeni, ukombozi ungekuwa mgumu kwayo kwa sababu masoko yana kumbukumbu ndefu ila ruwaza fupi. Hilo limelisaidia pakubwa bara hili.
Mfuko wa dola milioni 200 tuliouzindua kwa pamoja na Kamisheni ya Uchumi kwa Afrika ya Ãå±±½ûµØ(ECA) kusaidia utengenezwaji wa vifaa vya COVID ndani ya bara hili—vifaa vya kujilinda binafsi, barakoa kinga na vinginevyo vyote ulijumuishwa katika mfuko huo. Kama unakumbuka, wakati kama huu mwaka jana, kila mtu alikuwa aking' ang’ania vifaa hivi, na Afrika iliteseka. Kwa hivyo tulitoa ufadhili kwa kampuni kuelekeza upya viwanda kutengeneza barakoa kinga sahili na vifaa vya kujilinda binafsi.
Ìý
Ìý
Ìý