Addis Ababa/Geneva, tarehe 29 Novemba 2021: Kwa kuzingatia mafunzo tuliyoyapata kutokana na tajriba yetu ya pamoja ya msaada wa dozi za chanjo katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita, Shirika la Afrika la Upataji wa Chanjo (AVAT), Vituo vya Afrika vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (Africa CDC) na COVAX zingependa kutoa tahadhari kwa jamii ya kimataifa kuhusu hali ya msaada wa chanjo za COVID-19 kwa Afrika, na mataifa mengine yanayohusika katika COVAX, hasa yale yanayosaidiwa na Gavi COVAX Advance Market Commitment (AMC).
AVAT na COVAX zinajaliza juhudi za kila mmoja kusaidia nchi za Afrika kufikia malengo ya chanjo, kwa kutambua lengo la kimataifa la kuchanja asilimia 70 ya Waafrika. Msaada wa dozi za chanjo umekuwa chanzo muhimu cha usambazaji huku vyanzo vingine vikiimarika, lakini ubora wa msaada unapaswa kuimarika.
AVAT na COVAX zinalenga kuharakisha uafikiaji na usambazaji wa chanjo za COVID-19 barani Afrika. Kwa pamoja tunapanua usambazaji kwa haraka barani na kuzipa nchi usaidizi wa kuweza kutumia dozi wanazopokea.
Kufikia sasa, zaidi ya dozi milioni 90 zilizotolewa zimefikishwa barani kupitia COVAX na AVAT na mamilioni zaidi kupitia mipangilio baina ya nchi moja na nyingine.
Hata hivyo, misaada mingi? ya chanjo hadi sasa imekuja bila mpangilio, ikitolewa kwa ilani ya muda mfupi na yenye kipindi kifupi cha kutumika. Hii imesababisha changamoto kubwa kwa nchi kadhaa katika kupanga kampeni za chanjo na kuinua uwezo wa matumizi. Ili kufikia viwango vya juu vya chanjo katika bara zima, na ili misaada iwe chanzo endelevu cha usambazaji ambacho kinaweza kujaliza usambazaji kutoka kwa mikataba ya ununuzi ya AVAT na COVAX, hali hii lazima ibadilike.
Nchi zinahitaji usambazaji thabiti na unaotegemeka. Kupanga kwa ilani ya muda mfupi na kuhakikisha utumiaji wa dozi zenye kipindi kifupi cha matumizi kunazidisha sana mzigo wa mipango na vifaa kwenye mifumo ya afya ambayo tayari imelemewa.
Zaidi ya hayo, usambazaji usiotarajiwa wa namna hii hutumia uwezo - rasilimali watu, miundombinu, taratibu ya uhifadhi wa baridi - ambao unaweza kuelekezwa kwenye usambazaji fanifu wa muda mrefu na endelevu. Aidha usambazaji kama huo unazidisha kwa kiasi kikubwa hatari za kuisha kwa muda wa matumizi ya dozi hizi zilizo na kipindi kifupi cha matumizi zinapowasili nchini, na hili linaweza kuwa na athari za muda mrefu katika kuwa na uaminifu kwa chanjo.
Kuhusu Umoja wa Afrika
(UA) ni chombo cha bara kinachojumuisha Nchi 55 Wanachama zinazounda nchi za Bara la Afrika. Umoja wa Afrika ulizinduliwa rasmi mnamo 2002 kuchukua nafasi ya Shirika la Umoja wa Afrika (OAU, 1963-1999).
Kuhusu Kituo cha Kudhibiti Magonjwa cha Afrika (CDC)
Vituo vya Afrika vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (, ni taasisi maalum ya kiufundi ya Umoja wa Afrika ambayo inaimarisha nguvu na uwezo wa taasisi za afya ya umma za Afrika pamoja na ushirikiano wa kugundua na kukabiliana haraka na kwa ufanisi kwa vitisho na milipuko ya magonjwa, kwa misingi ya hatua na programu zinazoendeshwa kwa mujibu wa data. Jifunze zaidi hapa:?
Kuhusu Hazina ya Afrika ya Kupata chanjo (AVAT)
Hazina ya Afrika ya Kupata chanjo (AVAT) ni hazina maalumu iliyosajiliwa kule Mauritius. AVAT inafanya kazi kama wakala wa ununuzi kwa niaba ya Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (UA), ili kupata chanjo zinazohitajika na rasilimali za pamoja za ufadhili kwa ajili ya kufanikisha mkakati wa Afrika wa chanjo ya COVID-19 ambao unalenga kutoa chanjo kwa angalau 70% ya watu wa Afrika kulingana na mtazamo wa Afrika nzima.
AVAT ilianzishwa na Jopokazi la Upataji wa Chanjo ya COVID-19 la Afrika, lililoundwa mnamo Novemba 2020 na Rais Cyril Ramaphosa wa Jamhuri ya Afrika Kusini, katika wadhifa wake kama Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (UA), kama sehemu ya msaada wa Mkakati wa Chanjo ya COVID-19 ambayo iliidhinishwa na Ofisi ya Wakuu wa Nchi na Serikali wa UA mnamo Agosti 2020.
Taasisi kuu za washirika wa AVAT ni Vituo vya vya Afrika vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa vya Umoja wa Afrika (Africa CDC), Benki ya Uagizaji wa Bidhaa za Kiafrika (Afreximbank), na Tume ya Kiuchumi ya Umoja wa Mataifa ya Afrika (ECA).
Kuhusu COVAX
COVAX, nguzo ya chanjo ya?, inaongozwa kwa pamoja na CEPI, Gavi na WHO – ikifanya kazi kwa ushirikiano na UNICEF na PAHO kama washirika wa utekelezaji, watengenezaji wa chanjo wa mataifa yaliyostawi na yanayostawi, Benki ya Dunia, na wengine.
Ni mkakati wa pekee wa kimataifa ambao unafanya kazi na serikali na watengenezaji kuhakikisha kuwa chanjo za COVID-19 zinapatikana ulimwenguni kote kwa nchi zenye mapato ya juu na ya chini.
Misaada kwa COVAX, AVAT na nchi za Afrika lazima utolewe kwa njia inayoruhusu nchi kukusanya rasilimali za ndani kwa njia ifaayo ili kusaidia utoaji wa chanjo na kuwezesha upangaji wa muda mrefu wa kuongeza viwango vya utoaji wa chanjo. Tunatoa wito kwa jamii ya kimataifa, hasa wafadhili na watengenezaji, kujitolea kwa juhudi hii kwa kuzingatia viwango vifuatavyo, kuanzia tarehe 1 Januari 2022:
- Idadi na uthabiti: Nchi zinazotoa msaada zinapaswa kujitahidi kuachilia dozi zilizotolewa kwa wingi na kwa njia thabiti, ili kupunguza gharama za ununuzi. Tunatambua na kukaribisha hatua zinazofikiwa lakini kumbuka kuwa idadi ya vighairi kwa mtazamo huu inaweka mzigo kwa nchi, AVAT na COVAX.
- Kutengwa: Dozi hizi hazipaswi kutengwa ili kuwe na ufanisi mkubwa na kusaidia mpango wa muda mrefu. Utengaji unafanya iwe vigumu zaidi kugawa usambazaji kwa misingi ya usawa, na kuzingatia uwezo wa nchi mahususi wa matumizi ya chanjo. Pia unazidisha hatari kwa kuwa misaada yenye kipindi kifupi cha matumizi hutumia uwezo wa nchi wa uhifadhi wa baridi – na hivyo kufanya uhifadhi huo kutopatikana wakati ambapo AVAT au COVAX zinagawa dozi zenye muda mrefu wa matumizi chini ya makubaliano yao ya ununuzi.
- Muda wa matumizi: Kwa hivyo, dozi za msaada zinapaswa kuwa na muda usiopungua majuma 10 ya muda wa matumizi zinapofika nchini, kunaweza kuwa na ughairi pale ambapo nchi zinazopokea zinapoonyesha nia na uwezo wa kutumia dozi zenye muda mfupi zaidi wa matumizi.
- Ilani ya mapema: Nchi pokezi zinahitaji kufahamishwa kuhusu upatikanaji wa dozi za msaada mapema, kama majuma 4 kabla ya kuwasili kwa dozi hizo nchini.
- Muda makabilio:?Wadau wote wanapaswa kulenga makabilio ya haraka kuhusu taarifa muhimu. Hiyo inajumuisha taarifa muhimu za usambazi kutoka kwa watengenezaji (jumla ya kiasi kinachopatikana kwa msaada, muda wa matumizi, eneo la utengenezaji), uthibitisho msaada kutoka kwa wafadhili, na kukubalika/kukataliwa kwa mgao kutoka nchi mbalimbali. Taarifa za dakika za mwisho zinaweza kutatiza michakato zaidi, kuongeza gharama za ununuzi, kupunguza muda wa matumizi, na kuongeza hatari ya kufikia tarehe za mwisho wa matumizi.
- Vifaa vingine: Misaada mingi kufikia sasa haijumuishi vifaa vinavyohitajika vya chanjo kama vile sindano na vifaa vya kuchanganyisha chanjo, wala hailipi gharama za usafirishaji - ?kumaanisha kwamba misaada kama hii lazima itafutwe kivyake - hivyo basi kuleta gharama zaidi, utata na ucheleweshaji. Dozi za misaada zinapaswa kuambatanishwa na vifaa vingine vyote muhimu ili kuhakikisha usambazaji wa haraka na matumizi.
AVAT, Kituo cha Kudhibiti Magonjwa cha Afrika (CDC) na COVAX zimejitolea kushirikiana na nchi wafadhili, watengenezaji wa chanjo na washirika katika kuhakikisha viwango hivi vinazingatiwa, tunapoendelea kufanya kazi pamoja kufikia malengo ya chanjo ya Afrika.