Ãå±±½ûµØ

COP26 kuhusu hali ya hewa: Vipaumbele vya Bara Afrika

Get monthly
e-newsletter

COP26 kuhusu hali ya hewa: Vipaumbele vya Bara Afrika

— Bara linataka ushirikiano bora kuhusu mabadiliko na ufadhili.
Afrika Upya: 
15 July 2021
Mwanamke akitembea mashambani nchini Mali.
World Bank/Curt Carnemark
Mwanamke akitembea mashambani nchini Mali.
Ikiwa huwezi kusoma sasa, sikiliza tu toleo la sauti: 
Sauti ya Kiingereza

Mnamo tarehe 22 na 23 Aprili mwaka huu, Rais wa Marekani Joe Biden aliandaa Mkutano Mkuu wa Viongozi kuhusu Hali ya Hewa. Kulingana na Ikulu, mkutano huo mkuu ulilenga "kuchochea juhudi za chumi kuu ili kukabiliana na janga la hali ya hewa.'' Viongozi wa nchi 40, ikijumuisha nchi tano za Afrika, walishiriki katika mkutano huo kwa njia ya mtandao.

Tanguy Gahouma-Bekale
Bwana Tanguy Gahouma-Bekale, Mwenyekiti wa Kikundi cha Walioongoza majadiliano ya Afrika kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa chini ya UNFCCC.

Mkutano huo ulikuwa hatua muhimu, kabla ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa (UNFCCC) Mkutano wa Vyama (COP26), utakaofanyika jijini Glasgow mnamo Novemba hii.Ìý

Viongozi watano wa Afrika ambao walishiriki katika Mkutano Mkuu wa Viongozi walisisitiza wajibu wa lazima ambao bara hili lazima litekeleze katika juhudi za ulimwengu za kupunguza uzalishaji wa gesi chafu (GHG) na kupunguza joto duniani hadi 1.5C.ÌýWalikuwa Rais Félix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo; Ali Bongo Ondimba wa Gabon; Uhuru Kenyatta wa Kenya; Muhammadu Buhari wa Nijeria, na Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini.

Katika mkutano wa COP26, Kikundi cha wataalamu walioongoza majadiliano kutoka Afrika kitashikilia msimamo wa viongozi wa Afrika. Tutazungumza kwa sauti moja, thabiti na wazi huko Glasgow. Tutasisitiza kuwa COP26 itafaulu tu kama Afrika ikiwa kiini cha mazungumzo.ÌýKwa kweli, chini ya UNFCCC, kuweka Afrika katika kiini cha ajenda ya hali ya hewa ya ulimwengu ni wajibu wa lazima.

Hali ya Afrika inastahili uangalifu mkubwa: bara hili linachangia asilimia 4 tu ya jumla ya uzalishaji wa gesi chafu (GHG), kiwango cha chini zaidi kuliko eneo lingine lolote, lakini maendeleo yake ya kijamii na kiuchumi yanatishiwa na janga la hali ya hewa. Kwa maneno mengine, Afrika inachangia uzalishaji wa kiwango chini sana lakini ndiyo inayoathiriwa vibaya.

Kwa mfano, mbali na athari za janga la hali ya hewa kama ukosefu wa chakula, uhamiaji na uhaba wa maji, zaidi ya nusu ya nchi za Afrika huenda zikashuhudia mizozo inayohusiana na hali ya hewa.Ìý

Katibu Mkuu António Guterres akizungumza kwenye COP 26.
UN/Eskinder Debebe

Kulingana na Shirika la Mpango wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa, gharama za kila mwaka katika nchi zinazoendelea, ambazo kwa sasa zinakadiriwa kuwa dola bilioni 70, zitapanda hadi dola bilioni 300 ifikapo mwaka 2030 na dola bilioni 500 ifikapo 2050.

Wakati huo huo, serikali za Afrika kwa sasa zinatumia kati ya asilimia 2 - 9 ya Pato la Taifa kufadhili mipango ya ustahimilivu.

Mahitaji ya kipekee

Katika COP26 huko Glasgow, nchi zitazindua lengo la ustahimilivu na kupitisha mkakati wa kufikia lengo hili. Glasgow, kwa hivyo, inatoa fursa ya kutambua na kushughulikia mahitaji na hali za kipekee za Afrika. Kuna njia kadhaa za kufanya hivyo, ikijumuisha zifuatazo:

Kwanza, nchi zilizostawi lazima ziepuke kuhamisha wajibu wao wa hali ya hewa, hasa kuhusu uzalishaji wao wa jumla wa gesi chafu, kwa nchi zinazoendelea. Pia, uchumi uliostawi unapaswa kuongoza kwa malengo wazi ya kutozalisha gesi chafu kabisa kufikia 2050.Ìý

Pili, kulingana na ahadi na wajibu chini ya kifungu cha 4 cha UNFCCC, nchi zilizostawi lazima zitafute na kutoa rasilimali za kutosha za fedha za hali ya hewa na kusambaza teknolojia bora za mazingira katika nchi za Afrika.Ìý

Tatu, janga la COVID-19 halipaswi kulemaza ajenda ya fedha za hali ya hewa. Mwitikio ulioboreshwa na wenye maendeleo unahitajika kushughulikia janga la hali ya hewa, na fedha ndio kiini chake. Katika COP26, nchi lazima zikubaliane kuhusu mfumo wa kifedha, ikijumuisha makubaliano kuhusu kuendelea kwa ufadhili wa muda mrefu wa hali ya hewa (LTF) chini ya UNFCCC. Hii inafaa kujumuisha uzinduzi wa lengo jipya la kifedha chini ya Mkataba wa Hali ya Hewa wa Paris.

Wakuu wa Nchi za Afrika ambao walishiriki katika Mkutano Mkuu wa Viongozi kuhusu Hali ya Hewa, ulioongozwa na Rais wa Marekani, Joe Biden tarehe 22-23 Aprili 2021

  1. Rais Félix Tshisekedi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
  2. Rais Ali Bongo Ondimba, Gabon
  3. Rais Uhuru Kenyatta, Kenya
  4. Rais Muhammadu Buhari, Nijeria
  5. Rais Cyril Ramaphosa, Afrika Kusini

Nne, nchi zilizostawi lazima ziahidi kuziba pengo lao la kifedha la hali ya hewa kabla ya mwaka 2020 la dola bilioni 100. Dola bilioni 100 kwa mwaka zinapaswa kuwa kiwango cha chini kabisa, sio kiwango cha juu, na juhudi zinazoendelea lazima zifanyike kuamua na kukidhi mahitaji na vipaumbele vya nchi zinazoendelea.

Kwenye mkutano nchini Uingereza mwezi wa Juni, mataifa ya G7 yalitoa tena ahadi waliyotoa mwaka wa 2009 kuchangia dola bilioni 100 kila mwaka kusaidia nchi masikini kupunguza uzalishaji wa gesi chafu. Tangu 2009, hata hivyo, utafiti wa kisayansi unaonyesha kuwa bado mengi yanahitaji kufanywa katika kuzuia na ustahimilivu.

Tano, katika COP26, wanaoshiriki wa mazungumzo lazima watambue kwamba sehemu zenye masharti ya Michango Iliyoamuliwa Kitaifa (NDCs) zinawakilisha michango thabiti zaidi kwa Mkataba wa Paris kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, na hizi zinahitaji rasilimali za kifedha za hali ya hewa ambazo zinapaswa kupatikana kupitia makubaliano baina ya nchi mbili na yale ya nchi nyingi.Ìý

Mwishowe, Afrika inahitaji msaada wa ziada kwa mipango yake, ikiwemo Mpango wa Nishati Mbadala wa Afrika (AREI) na Mpango wa Ustahimilivu wa Afrika (AAI).ÌýBara hili linahitaji misaada, sio tu mikopo inayozidisha mzigo wake wa deni. Kuongezeka kwa deni na janga la COVID-19 kumedhoofisha uwezo wa nchi masikini kukabiliana na janga la hali ya hewa.

Vipaumbele vyetu

Kwa jumla, vipaumbele vya Afrika kwa COP26 vinajumuisha ustahimilivu, fedha za hali ya hewa, mkakati wa soko (Kifungu cha 6), mkakati wa uwazi, kutimiza ahadi za uzuiaji kabla ya 2020 na kutambua mahitaji na hali za kipekee za Afrika.Ìý

Mikakati ya soko chini ya Mkataba wa Paris inapaswa kusaidia kuinua hamu ya kutekeleza hatua za kuzuia, kusaidia maendeleo endelevu ya kijani katika nchi za Afrika na kutoa fedha za ustahimilivu.Ìý

Kwa bahati mbaya, mkakati wa uwazi wa Mkataba wa Paris haukuwa na lengo katika COP25. Unapaswa kuzungumziwa katika COP26.ÌýÌý

Mkakati wa uwazi unapaswa kuangazia maendeleo na mafanikio katika vitendo na usaidizi; unapaswa kuwa zana ya kuongeza hatua za hali ya hewa na matamanio huku ukisaidia nchi zinazoendelea kujenga na kudumisha mifumo ya uwazi ya kitaifa kukidhi mahitaji ya kuripoti yaliyotajwa katika Mkataba wa Paris.

Aidha, kunapaswa kuwa na ongezeko la msaada wa kimataifa kwa mikakati na ustahimilivu barani Afrika. Kupungua kwa sasa kwa msaada rasmi wa maendeleo na nchi zilizostawi kutapunguza uwezo wa nchi masikini kupambana na janga la hali ya hewa.

Tuko karibu na dharura ya hali ya hewa; kwa hivyo, uangalifu na rasilimali kama zinazoelekezwa kwa COVID-19 zinapaswa pia kutumiwa kukabiliana na tishio la mabadiliko ya hali ya hewa. Kama vile janga la COVID-19, mabadiliko ya hali ya hewa hayana mpaka. Kwa Afrika, janga hili limeleta fursa ya kipekee kwa urejesho wa usafi wa anga.Ìý

Kikundi cha Afrika kilitumia fursa ya vikao vya mashirika tanzu ya Umoja wa Mataifa ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa (SBs), yaliyofanyika kutoka tarehe 31 Mei hadi tarehe 17 Juni 2021, kusisistiza nafasi zao katika masuala anuwai. Vikao vya mashirika tanzu wakati wa au kabla ya Glasgow vinaweza kuwa muhimu kuwezesha vipaumbele vya mada za ajenda zinazohusu ustahimilivu, uhamishaji wa teknolojia, miongoni mwa nyingine.

Itakuwa awamu ya Afrika kuwa mwenyeji wa COP27. Itafanyika Novemba 2022 nchini Misri. Mafanikio ya COP26 yataipa Afrika taarifa muhimu inapojiandaa kwa COP inayofuata.Ìý

Afrika ina hamu ya kushirikiana na nchi zilizostawi ili kuhakikisha matokeo bora katika COP26. Hatuwezi kukubali kushindwa.

BwanaÌýGahouma-BekaleÌýni Mwenyekiti wa Kikundi cha Walioongoza majadiliano ya Afrika kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa chini ya UNFCCC.

More from this author