Dau la plastiki latia nanga mji mkongwe Zanzibar
Get monthly
e-newsletter
Dau la plastiki latia nanga mji mkongwe Zanzibar
Hatimaye dau la plastiki lililosafiri kilometa 500 kutoka Lamu, nchini Kenya hadi Mji Mkongwe, Zanzibar nchini Tanzania limetia nanga Unguja likiwa limetimiza azma yake ya听 kuelimisha jamii zilipo pwani kwa Kenya na Tanzania kuhusu madhara ya plastiki kwa binadamu, mazingira na viumbe vya majini.听
Likiwa limebeba wanamazingira kutoka shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP na kampuni iliyohusika na ujenzi, Flipflopi, dau hilo lilipata fursa kuhamasisha jamii hizo za pwani juu ya madhara ya plastiki.
Walikutana na wanafunzi, wanajamii na viongozi wa serikali na kubadilishana mawazo kuhusu jinsi ya kubadili mtazamo wa matumizi ya plastiki.
Akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa baada ya dau hilo kutia nanga mji mkongwe, Mwakilishi wa shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP nchini Tanzania, Clara Makenya amesema..
(Sauti ya Clara Makenya)
Na le lengo la safari limetimia
(Sauti ya Clara Makenya -2)
Dau hilo lililojengwa na Ali Skanda kwa tani elfu 10 za taka za plastiki lilianza safari yake tarehe 24 mwezi Januari huko Lamu, nchini Kenya na kupitia Kipini, Malindi,Watamu, Kilifi, Mombasa, Diani, Shimoni, Wete, Pemba Kusini, Nungwi na hatimaye 听leo 听tarehe 7 limetia nanga Mji Mkongwe Zanzibar.