Ripoti mpya ya shirika la afya duniani, WHO,听听imesema kuwa watu wengi zaidi walipata tiba dhidi ya ugonjwa wa Kifua Kikuu, TB, mwaka 2018 kuliko wakati wowote ule kutokana na kuimarika kwa mbinu za utambuzi wa ugonjwa huo.听听
听kupitia ripoti hiyo iliyozinduliwa leo mjini Geneva, Uswisi na Washington DC nchini Marekani, inasema kuwa duniani kote watu milioni 7 waliugua na kutibiwa TB ikiwa ni ongezeko kutoka wagonjwa milioni 6.4 mwaka uliotangulia wa 2017.
Ripoti hiyo imesema hali hiyo imewezesha dunia kufikia lengo la azimio la kisiasa la kuhusu kutokomeza TB.
Pamoja na hayo, mwaka 2018 ulishuhudia pia kupungua kwa vifo vitokanavyo na TB kutoka milioni 1.6 mwaka 2017 hadi milioni 1.5 mwaka jana.
Hata hivyo ripoti hiyo inasema kuwa mzigo wa Kifua Kikuu听听unasalia mkubwa kwa nchi za kipato cha chini na jamii zilizo pembezoni ambako mwaka jana pekee watu milioni 10 waliambukizwa ugonjwa huo wa Kifua Kikuu.
Akizungumzia ripoti hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema,听听鈥渓eo hii tunaadhimisha kuvuka lengo la kihistoria la kufikia watu ambao awali walikuwa hawafikiwi na huduma za kinga na tiba dhidi ya TB.鈥
Dkt. Tedros amesema hatua ya leo ni dhahiri kuwa听鈥渢unaweza kufikia malengo ya kimataifa iwapo tutafanya kazi pamoja kama tulivyofanay kupitia mpango wa Baini, Tibu wote, Tokomeza TB, mpango ambao ni wa WHO, ubia wa kutokomeza TB na fuko la kimataifa la kutokomeza Ukimwi, TB na Malaria.鈥
Hata hivyo ripoti hiyo inasema bado wagonjwa milioni 3 wa TB hawajapata huduma inayotakiwa.
Dhima ya huduma ya afya kwa wote
WHO inasema katika mataifa menig, mifumo dhaifu ya afya na uhaba wa watendaji kwenye sekta ya afya vimekwamisha upimaji wa wakati na tiba sahihi dhidi ya TB.
鈥淢ifumo dhaifu ya utoaji wa taarifa ni tatizo lingine. Watoa huduma wa afya wanaweza kutibu watu lakini iwapo wanatashindwa听听kutoa ripoti sahihi kwa mamlaka za kitaifa, wanakuwa wameacha taswira sahihi ya ugonjwa,鈥澨imesema WHO.
Halikadhalika mzigo听听unasalia pia kwa mgonjwa听听ikilezewa kuwa takribani asilimia 80 ya wagonjwa wa TB kwenye nchi za kipato cha chini wanatumia zaidi ya asilimia 20 ya kipato cha mwaka cha kaya kutibu ugonjwa huo.
鈥淢aendeleo endelevu katika tiba dhidi ya TB yanahitaji mifumo thabiti ya afya na watu kuweza kufikia huduma kwa urahiai. Hii ina maana kupanga upya uwekezaji katika huduma ya msingi ya afya na kutekeleza ahadi ya huduma ya afya kwa wote,鈥澨amesema Dkt. Tedros.
Mwezi uliopita, wakuu wa serikali walikubaliana juu ya azimio la huduma ya afya kwa wote, UHC ambalo linaangazia umuhimu wa kupanua huduma za msingi za afya ili ziweze kujumuisha pia magonjwa ya kuambukiza kama vile Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria.
Usugu wa dawa dhidi ya TB
Tatizo lingine kwenye Kifua Kikuu ni usug uwa dawa ambapo mwaka 2018, kulikuwepo na wagonjwa tarkibani 500,000 ambao ugonjwa huo haukutibika na dawa zilizopo.
WHO inasema kuwa mwongozo wake mpya unalenga kuboresha tiba dhidi ya usugu wad aw kwa kubadili听听tiba iwe ni ya dawa za kunywa pekee na zilizo salama na fanisi.
Akizungumzia hali hiyo, Dkt. Tereza Kasaeve, mkuu wa Idara ya TB kwenye WHO, amesema,听鈥淲HO听听inashirikiana na nchi, wadau na mashirika ya kiraia kuchagiza utabibu wa TB na tunashirikiana na sekta zote ili hatimaye tuweze kupata jawabu la ugonjwa huu hatari na kuokoa maisha.鈥
Ufadhili bado kizungumkuti
Mapambano dhidi ya TB yanahitaji fedha na hadi sasa ukata ni tatizo ambapo WHO inakadria kuwa pengo kwa tiba na huduma mwaka huu ni dola bilioni 3.3
Fahamu kuhusu TB
TB ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria Mycobacterium tuberculosis ambaye mara nyingi huathiri mapafu. Hata hivyo ugonjwa huu unazuilika na unatibika.
Takribani robo ya wakazi wa dunia wamekumbwa na bakteria huyo lakini si wagonjwa na hawawezi kuambukiza mtu mwingine.
Mataifa yaliyokuwa yana wagonjwa wengi wa TB mwaka 2018 ni China, India, Indonesia, Nigeria, Pakistan, Ufilipino na Afrika Kusini.
Hata hivyo mataifa kama vile Brazil, China, Urusi na Zimbabwe ambayo yote yana mzigo mkubwa wa wagonjwa, yalifikia kiwango cha matibabu kwa zaidi ya asilimia 80.