缅北禁地

Ni nani anawalinda watu wenye ulemavu dhidi ya COVID-19? -Mtaalamu wa UN

Get monthly
e-newsletter

Ni nani anawalinda watu wenye ulemavu dhidi ya COVID-19? -Mtaalamu wa UN

缅北禁地News
19 March 2020
Catalina Devandas
缅北禁地Photo/Manuel Elias
Catalina Devandas

Mtaalamu听maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu wenye ulemavu, Catalina Devandas, hii leo mjini Geneva ameonya kwamba juhudi kidogo sana zimefanywa kuwapa maelekezo na usaidizi unaohitajika, watu wenye ulemavu ili kuwalinda wakati wa mlipuko huu wa ugonjwa wa听COVID-19听ingawa wengi wao wako katika kundi la wale walioko hatarini zaidi.

鈥淲atu wenye ulemavu wanajihisi kuwa wameachwa nyuma. Hatua kama kujitenga au kukaa umbali kati ya mt una mtu kunaweza kusiwezekane kwa wale ambao wanaishi kwa kutegemea msaada wa watu wengine kula, kuvaa na kuoga. Msaada huu ni wa msingi kwa maisha yao na mataifa yanapaswa kuchukua hatua zaidi za ulinzi wa jamii ili kuhakikisha msaada endelevu katika hali salama hadi mwisho wa janga.鈥听Amesema Bi Devandas.

Mtaalamu huyo wa Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa hatua za makusudi ni muhimu kuwafanya watu wenye ulemavu waweze kupunguza kukutana na watu na hatari ya kuambukizwa. Wanatakiwa kuruhusiwa kufanya kazi kutokea nyumba au kupatiwa likizo za malipo ili kuwahakikishia uhakika wa kipato. Pia ewana familia na wasaidizi wanaweza kutakiwa kuangaliwa ili waweze kuendelea kutoa msaada kwa watu wenye ulemavu katika kipindi hiki cha听COVID-19.

鈥淯wezekano wa kupata msaada wa kifedha ni muhimu pia ili kupunguza uwezekano wa watu wenye ulemavu na familia zao kuangukia katika hatari zaidi au umaskini. Watu wengi wenye ulemavu wanategemea huduma ambazo zimeahirishwa na wanaweza wasiwe na fedha ya kutosha kuhifadhi vyakula na dawa au kumudu gharama za ziada za kuletewa huduma nyumbani.鈥听Amefafanua.

Mtaalamu huyo wa Umoja wa Mataifa ameeleza pia kuwa ni muhimu kampeni kwa umma na taarifa kutoka katika mamlaka za kiafya za nchi, ni lazima zitolewe kwa umma kwa njia ya lugha ya alama na namna ambayo zinaweza kupatikana kwa kila mtu ikiwemo teknolojia ya kidijitali, sauti kuwekewa maandishi, ujumbe mfupi wa simu, lugha rahisi na inayosomeka kirahisi.

鈥淢ashirika ya watu wenye ulemavu yanapaswa kuhusishwa na kuombwa ushauri katika hatua zote za kupambana na COVID-19.鈥听Amehitimisha Bi Devandas.