Mikakati ya kutaka watu kubaki majumbani ili kuzuia kuenea kwa virusi vya ugonjwa waCoronaau COVID-19 imewaweka wafanyakazi njia panda akiwa hafahamu achague afe njaa na familia yake au afe kwa virusi.
Mikakati ya kutaka watu kubaki majumbani ili kuzuia kueneakwavirusivya ugonjwa wa CoronaauCOVID-19 inatishia kuongezakwaasilimia 56 viwango vya umaskini miongoni mwa wafanyakazi wa sekta isiyo rasmi walioko nchi za kipato cha chini.
Shirika la kazila Umoja wa Mataifa,limesema hayo katika nyaraka yake mpya wakati huu ambapo mataifa kadhaa yamechukua hatua kali kuzuia watu kutoka majumbani ikiwemo hata kufanya biashara ndogo ndogo kamanjiaya kudhibiti COVID-19.
ILOinaesema kiwango hicho cha ongezeko la umaskinikwaasilimia 56 kati nchi hizo za kipato cha chini ni kikubwa ukilinganisha na asilimia 52 nchi za kipato cha juu na asilimia 21kwawalioko nchi za kipato cha kati.
Shirika hilo linasema kuwa,“takribani wafanyakazi bilioni 1.6 wa sekta isiyo rasmi kati ya wafanyakazi bilioni 2 wa sekta hiyo duniani kote, wameathiriwa na hatua za kukaa ndaniaukutotembea hovyo. Wengi wao wako kwenye sekta zilizoathiriwa zaidiaukwenye maeneo ambayo kuna madhara makubwa. Sekta hizo ni pamojana zile za malazi, chakula, uzalishaji, biashara ya jumla na rejareja na zaidi ya wakulima milioni 500 wanaozalisha chakulakwaajili ya wakazi wa mijini.”
Ripoti inasema kuwa wanawake ndio wamekumbwa zaidi kwenye sekta hizo na kwamba,“wakati wafanyakazi wakihitaji kufanya kazi kulisha familia zao, hatua za kudhibiti COVID-19 katka nchi nyingi haziwezi kutekelezwa ipasavyo. Hii inaathiri juhudi za serikali za kulinda jamii na kukabiliana na janga.”
Kama hiyo haitoshi,ILOinasema mvutano huo unaweza kuleta mvurugano katiika nchi ambako sekta isiyo rasmi ni kubwa.
“Wafanyakazi wa sekta isiyo rasmi wakiwa hawana mbinu yoyote ya kusaidia familia zao, wanabakia kwenye mkanganyiko, wafekwanjaaaukwavirusi,”imesema ripoti hiyo ikiongeza kuwa hali inakuwa mbaya kutokana na kuongezekakwauhaba wa chakula ambao unakumba zaidi wale waliokuwa kwenye sekta isiyo rasmi.
Ikimulika wafanyakaiz wa ndani, ripoti inasema kuwakwawafanyakazi hao milioni 67 ambao asilimia 75 kati yao wako kwenye sekta isiyo rasmi, suala la ukosefu wa ajira limekuwa tishio kama vilivyovirusivyenyewe vya Corona.
“Wengi wao hajawaweza kufanya kazi, iwekwaombi la waajiri waoaukwazuio la kudhibiti kueneakwaCorona. Wale ambao wanaendelea na ajira, wako hatarini zaidi kuambukizwa Corona wakihudumia familia kwenye makazi binafsi.Kwawafanyakazi wa ndani wahamiaji milioni 11 hali ni mbaya zaidi,”imesema ripoti hiyo.
Akizungumzia ripoti hiyo, Philippe Marcadent, Mkuu wa kitengo cha sekta isiyo rasmi,ILOamesema kuwa,“Janga la COVID-19, linaongeza ukosefu wa usawa ambao tayari ulikuwepo. Hatua za kisera lazima zihakikishe msaada unafikia wafanyakazi na kampuni zenye uhitaji zaidi.”
Kimaeneo, hatua za kuzuia watu kutochangaman zimekuwa na madhara zaidi huko Amerika ya Kusini ikifuatiwa na nchi za kiarabu, halafu Afrika, kisha Asia na Pasifiki na Ulaya na Asia ya Kati.
ILOinapendekeza kuwa nchi zinapaswa kufuata mkakati mchanganyiko unaozingatia athari zote za kiafya na kiuchumi.
Kwamantiki hiyo, nchi zinatakiwa kuwa na sera zinazopunguza fursa za wafanyakazi wa sekta isiyo rasmi kupata maambukizi yavirusi, kuhakikisha wale wanaoambukizwa wanapata huduma ya afya, kuwapatia msaada wa kipato na chakula wao na familia zao pamoja na kuzuia hali ya sasa isilete madhara ya kudumu ya kiuchumi.