缅北禁地

Mtoto wa miaka 4 anajisiwa Somalia, UNFPA yazungumza

Get monthly
e-newsletter

Mtoto wa miaka 4 anajisiwa Somalia, UNFPA yazungumza

缅北禁地News
18 May 2020
Wasichana wakiwa katika kibanda cha walionyanyasiwa kijinsia Mogadishu. Baaadhi wanaweza kupata ajira katika duka mama mmoja mjini humo la vitambaa.
UNICEF/Holt
Wasichana wakiwa katika kibanda cha walionyanyasiwa kijinsia Mogadishu. Baaadhi wanaweza kupata ajira katika duka mama mmoja mjini humo la vitambaa.

Taarifa ya UNFAPA iliyotolewa leo mjini Mogadishu, Somalia, inasema kuwa mtoto huyo wa kike alifanyiwa kitendo hicho tarehe 14 mwezi huu wa Mei huko Madina mjini Mogadishu.

鈥淭unalaani vikali kitendo cha kunajisiwa mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 4. Tunalaani vikali ukatili huu wa kingono wa kutisha. Ni kwa masikitiko makubwa tunaendelea kushuhudia visa vya aina hii nchini Somalia,鈥听imesema taarifa hiyo.

Shirika hilo limesema linasimama kwa mshikamano na familia ya mtoto huyo, 鈥渘a tunatoa wito kwa mamlaka kuongeza kasi ya uchunguzi wa kisa hiki na tunatoa wito ufanyike mchakato sahihi wa kimahakama.鈥

Halikadhalika听听imesisitiza wito wake wa kutaka kupitishwa na kuwa sheria kwa muswada wa sheria ya makosa ya ukatili wa kingono, muswada ambao imesema umesalia bungeni muda mrefu bila kupitishwa.

鈥淯NFPA Somalia inatoa wito wa kuimarishwa kwa mifumo ya ulinzi wa wanawake na watoto ambao wameendelea kuwa hatarini kukumbwa na ukatili wa kijinsia,鈥听imesema taarifa hiyo ikitamatisha kuwa leo na kila siku,听鈥渉ebu na tutetee haki za binadamu, usalama na utu wa kila mwanamke na kila mtoto wa kike popote pale alipo.鈥