Mlipuko wa virusi vya Corona au听听kwa kiasi kikubwa umeathiri kila nyanja ya maisha ya watu duniani kote ukiacha kwamba umesababisha mamilioni ya vifo lakini pia umeathiri uchumi na maisha ya kijamii.
Na athari hizo za kijamii ni pamoja na watu kupoteza pato la familia kutokana na kukpoteza ajira, watoto kushindwa kuhudhuria masomo na hata shughuli za ujasiriliamali kusambaratika hali ambayo imewafanya wengi kujikuta katika wakati mgumu kumudu maisha ya kila siku.
Lakini si kwa mjasiriliamali wa ufundi cherahani Beatrice Mbugi kutoka Mbeya Tanzania aliyeanza kazi hiyo ya ushoni tangu mwaka 1998, janga hili la corona limempa mwelekeo mpya wa kazi yake ya ujasirilamali.
Jina langu ni Beatrice Teso Mbugi, fundi wa kushona ninaishi kata ya Nzove Mbeya Tanzania.Hii kazi naipenda sana na nimejifunza mwaka wa 1998 lakini kwa kipindi hiki sasa cha huu ugonjwa听 ulioingia cha ukweli ni kwamba imekuwa ni changamoto kwa wateja wetu ambao wanashona nguo kwa vile hawaji na hawawezi kusema wanunue vitenge au vitambaa waje听 washone kwangu nguo. Ila wanajifungia ndani na kuwaza namna gani watajikinga听 na ugonjwa huu wa corona.
Hivyo basi nami kama fundi nimetumia fursa hii na kujiongeza, nimejiongeza nashona barakoa za kutosha. Hizi barakoa ni za kitambaa ambazo unaweza kuzitumia, ukafua vizuri na kuzinyosha vizuri tofauti na zile ambazo zinavaliwa masaa manne .
Nilifika katika hospitali ya rufaa Mbeya nilifika pale na kukuta kweli wajasiriamali wameshona barakoa nyingi na kwa kweli mtu anakuwa na shida ya kuingia hospitalini na kuhudumiwa basi inabidi tu achukue lakini mimi niliangalia kiwango cha zile barakoa tunazoletewa za misaada nikaangalia mfumo na muundo wa ile barakoa nikaona nitengeneze ya kitambaa lakini pia nitengeneze ya听 sponji kama hii ambayo inaendana kabisa na ile kama ya msaada.
Pamoja na kuleta adha听COVID-19听pia imenisadia silali njaa:Fundi Beatrice