Utunzi wa mazingira ni moja ya malengo makuu ya Umoja wa Mataifa.
Lakini dini inachukua nafasi gani katika kuwashauri waumini kuwa katika mstari wa mbele katika utunzaji wa mazingira. Shirika la WafransiskoWakapuchini ambalo liko chini ya kanisa na katoliki nimoja ya mashirika ambayo yako katika mstari wa mbele kutunza mazingira kwa ushirkiano na shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa. Mwandishi wa Nairobi, nchini Kenya, JasonNyakundialihudhuria sherehe za kanisa hilo zilizofanyika Nairobi na kuzungumza na Brother Benedict Ayodi, ambaye pia ni Mkurugenzi wa vuguvugu la mazingira la kanisa katoliki barani Afrika.
Sherehe ya leo ni kama kuweka ishara ya kuonyesha kwamba tumemaliza miaka mitano tangu baba Mtakatifu atoe barua yake ya Udatusina pia ni kuwahimiza hasa zaidi ndugu na dada zetu hasa wakatoliki na hata waleambaosi wakatoliki kwamba lazima tulinde mazingira. Hii ni kama ishara ya vitendo lakini anawahimiza wengine pia wafanye hivyo na watunze mazingira kwa njia moja au nyingine
Mnaushirikiano upi naShirika la Umoja wa Mataifa la kulinda Mazingira ?
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira UNEPlililopohapa Nairobi tunaambiwa kwamba nishirikala kipekee lililoko hapa Afrika na kwa hivyo tunashirikiana kwa karibu sana kwa sababu Umoja wa Maitafa una kitengo kinachoitwa Faith and Earth-yaani imani na mazingirahivyo basi sisi tunashirikiana nawao kwa vile wanajua kwamba wale watu ambao wanaeneza Imani wana watu wengi pia ambao wakionyeshwa mifano na kusaidiwa wanaweza chukua hatua kwa kulinda mazingira ya Climate Action and Climate Justice
Kwa maoniyako unafiriki Dini inastahili kuchukua nafasi gani katika kulinda mazingira?
Katika Bibilia na pia katika Koran tukufu tunajua kwamba mwanzoni mungu aliumba mazingira hivyo basi akatuweke kamawakristovile ambavyowakristowanaamini kwamba alituweka katika lile shamba la Eden,hivyo basi sisi watu wa imani tunaambiwa kwamba lazima tuwe watu ambao wanatunza vyema mazingira kwa vile mwishoni tutatoa hesabu kwa mungu jinsi tulivyo fanya jukumu letu la kulinda mazingira hivyo basi ni Imani yetu na pia sio tu kwa sababu ya Imani. Mtakatifu Francisco amabye sisi tunamfuata kama kapuchini wa Francisco aliishi miaka 800 iliyopita kule Asizi Italia na kule tunaambiwa kwamba alianza kumshukuru mungu na ndipo sasa hata hilo jina la Udatusi Praise God likaja ama tumshangilie mungu kwa sababu ametupa mazingira