Wanawake ikiwemo wajawazito ni walengwa wa ukatili wa kingono Sudan Kusini-Ripoti
Get monthly
e-newsletter
Wanawake ikiwemo wajawazito ni walengwa wa ukatili wa kingono Sudan Kusini-Ripoti
Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo inaonyesha ongezeko la ukatili wa kingono katika jimbo la Unity kaskazini mwa 听Sudan Kusini, ikisema wanawake 134 na wasichana wamebakwa na wengine 41 wamekumbwa na aina nyingine za ukatili wa kingono kati ya Septemba na Disemba 2018.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi, msemaji wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu,OHCHR,听 Rupert Colville amesema, miongoni mwa manusura ni watoto wa umri wa miaka nane, huku idadi kamili ya visa hivyo ikitarajiwa kuwa juu zaidi ya visa vilivyoripotiwa.
Ripoti hiyo iliyotolewa kwa pamoja na OHCHR na Ujumbe wa Umoja huo nchini Sudan Kusini, UNMISS inaonya kuwa licha ya mashambulio dhidi ya raia kupungua kwa kiasi kikubwa tangu kutiwa saini makubaliano ya amani lakini ukatili wa kingono unaendelea kutekelezwa katika jimbo la Unity Kaskazini.
(Sauti ya Rupert)
鈥淎silimia 87 ya wanawake na wasichana walibakwa na zaidi ya mtu mmoja听 kwa saa nyingi. Miongoni mwa watu waliobakwa, 50 walikuwa ni watoto huku mtoto mmoja akiwa na umri wa miaka nane, wanawake wajawazito na wanawake wanaonyonyesha pia walilengwa. Katika kisa kimoja Disemba 17 mwaka jana, kijiji cha Langa kaskazini mwa Bentiu, wanawake watano walibakwa ambapo wanne kati yao walikuwa na uja uzito mmoja akiwa karibu miezi tisa na mwingine miezi saba.鈥
Ofisi ya haki za binadamu 听imesema uchunguzi umeonyesha kuwa kuna mambo mbali mbali yamechangia hali hiyo ikiwemo idadi kubwa ya wapiganaji wanaosubiri utekelezaji wa makubaliano ya amani, uwepo wa idadi kubwa ya vijana wa makundi yaliyojihami na ukosefu wa uwajibishwaji katika matukio ya ukatili wa kingono hapo awali.
Collive ameongeza kuwa
(Sauti ya Rupert Colville]
鈥淜amishna mkuu Michelle Bachelet ametoa wito kwa mamlaka nchini Sudan Kusini kuchukua hatua ikiwemo zilizoorodheshwa kwenye makabaliano ya amani, lkulinda wanawake na wasichana, kuchunugza kwa haraka madai ya ukatili wa kingonoi na kuwawajibisha washukiwa kwa njia ya kisheria.鈥
Kufuatia ongezeko la ripoti za ukatili wa kingono, UNMISS iliwasiliana na serikali na kuongeza doria na kuweka mahakama ya muda katika maeneo ya hatari ikiwemo Bentiu na Malakal.