Mamilioni yaahidiwa katika hafla ya kuongeza kasi ya Afrika kukabiliana na tabianchi

Get monthly
e-newsletter

Mamilioni yaahidiwa katika hafla ya kuongeza kasi ya Afrika kukabiliana na tabianchi

Uingereza iliahidi dola milioni 230, Uholanzi dola milioni 110, AfDB dola bilioni 12.5, Ujerumani kuongeza mchango hadi dola bilioni 6 ifikapo 2025
Kingsley Ighobor
Afrika Upya: 
8 Novemba 2022
山Climate Change
Leaders and heads of international organisations hold hands before start of the event.

Wakati Kristalina Georgieva, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), alipotakiwa kutoa maoni yake katika hafla kuhusu Afrika kwenye mkutano wa COP27 uliokuwa ukiendelea huko Sharm El Sheikh, alianza kwa kuitaka hadhira kubwa kuipigia Misri na Afrika makofi.

Afrika imezingirwa; Afrika haiwezi kukimya. Tunatafuta ushirikiano. Megawati za maneno lazima zitafsiriwe kuwa megawati za ufadhili kwa Afrika.
Mr. Akinwumi Adesina
Rais wa Africa Development Bank (AfDB)

Na kisha, akiinua mikono yake kuunda ishara ya moyo, Bi. Georgieva alitangaza: "Tunaahidi moyo wetu kwa Afrika."

Alikuwa akizungumza katika hafla ya Kuongeza Kasi ya Afrika Kukabiliana na hali ambapo tamasha la mapenzi liliendelea na kila kauli ya viongozi wa dunia au wawakilishi wao, ikiwa ni pamoja na ya Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Uingereza, James Cleverly, ambaye alisema alihitaji kuungama hadharani.

"Mama yangu alitoka Sierra Leone, alitangaza. "Tafadhali nisamehe ikiwa nitadumisha makini ya kibinafsi barani Afrika." Alisema nchi yake ina makini sawia kwa maendeleo ya Afrika.

Hafla hiyo haikuhusu tu hotuba; mamilioni ya dola yaliahidiwa kuunga mkono Mpango wa Afrika Kuongeza Kasi ya Kukabiliana na hali () (AAAP) - mpango unaoongozwa na Afrika wa kukabiliana na hali unaolenga kupunguza hatari ya mabadiliko ya tabianchi kwa kukabiliana vyema.

Ahadi

Uingereza iliahidi pauni milioni 200 (karibu dola milioni 230) na itaongeza mara tatu ufadhili wake wa kukabiliana na tabianchi kutoka pauni milioni 500 hadi pauni bilioni 1.5 ifikapo 2025.

Uholanzi itatoa dola milioni 110 kwa AAAP.

Ujerumani itaongeza mchango wake wa tabianchi hadi dola bilioni 6 kwa mwaka ifikapo 2025. Takriban nusu ya ufadhili huo utalenga kukabiliana na hali hiyo, ikiwa ni pamoja na katika Afrika.

Marais Macky Sall wa Senegal (pia Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika), Nana Akufo-Addo wa Ghana, William Ruto wa Kenya, Andry Rajoelina wa Madagascar, Hassan Sheikh Mohamed wa Somalia, walikuwa kwenye hafla hiyo.

Walikuweko pia Chansela Olaf Scholz wa Ujerumani na Waziri Mkuu Mark Rutte wa Uholanzi, miongoni mwa wengine.

Kiini ni hali mbaya ya mabadiliko ya tabianchi barani Afrika, iliyozidishwa na athari za mzozo wa Ukraine na janga la COVID-19.

Rais wa Africa Development Bank (AfDB), Akinwumi Adesina, alisisitiza haja ya kukabiliana na hali hiyo kwa ufanisi barani Afrika. Mada iliyokaririwa katika hafla hiyo ilikuwa ufadhili wa kutosha wa miradi inayohusiana na tabianchi.

Bi. Georgieva alisema “Bila msaada, Afrika haitatimiza uwezo wake. Sharti kila mmoja wetu asimame na kuhesabiwa.”

Bw. Cleverly wa Uingereza alisisitiza: "Lazima tutimize ikiwa Afrika itashinda mabadiliko ya tabianchi na kutimiza uwezo wake usio na kikomo."

Bila msaada, Afrika haitatimiza uwezo wake. Sharti kila mmoja wetu asimame na kuhesabiwa
Ms. Kristalina Georgieva
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF)

Kwa Bw. Scholz, kulikuwa na dharura fulani: Alisema "Muda unayoyoma" kwa mataifa yaliyoendelea kiviwanda kutimiza ahadi yao ya ufadhili wa tabianchi wa $ bilioni 100 ifikapo 2025, akiongeza kuwa Afrika ilikuwa inachangia uzalishaji wa gesi hatari kwa kiwango kidogo mno.

Wito wa pamoja

Viongozi wa Afrika waliungana katika wito wao wa msaada wa kifedha. Hivi sasa, alilalama Rais Sall, mataifa mengi ya Afrika yanakopa ili kufadhili miradi ya kukabiliana na hali hiyo, akitoa mfano wa miradi ya treni ya umeme na mabasi ya Senegal inayogharimu $ bilioni 1.4.

Rais Akufo-Addo (Ghana), pamoja na Rais Ruto (Kenya) walisema Afrika inahitaji sindano ya haraka ya ufadhili wa kukabiliana na hali hiyo.

Ni lazima uwe wa “kutosha, kwa wakati unaofaa na upatikane ili uwe na ufanisi,” alisema Bw. Ruto.

Kusaidia Afrika kuimarisha mazoea ni "sharti la kimaadili," Bw. Adesina alidumisha.

Yalikuwa pia maoni ya Patrick Verkooijen, Afisa Mkuu Mtendaji wa , shirika la kimataifa linalotoa huduma za uwakala kutoa suluhu ili kusaidia kukabiliana na hali hiyo.

Mbali na athari nyingi mbaya za mabadiliko ya tabianchi, mkuu huyo wa AfDB alilalamika kuwa Waafrika wapatao milioni tano walitoroka makazi yao.

“Afrika imezingirwa; Afrika haiwezi kukimya. Tunatafuta ushirikiano,” alisema Bw. Adesina. Aliongeza: “Viongozi wa dunia wanahitaji kusikia sauti zetu. Megawati za maneno lazima zitafsiriwe kuwa megawati za ufadhili kwa Afrika.

Mahitaji ya ufadhili ya Afrika

Wakati Afŕika inahitaji dola bilioni 33 kila mwaka kukabiliana na hali hiyo, kwa sasa inapokea kaŕibu dola bilioni 6, na kuwafanya viongozi wa Afŕika kuunga mkono AAAP.

Chini ya mwamvuli wa AAAP, AfDB na GCA zinatumai kukusanya dola bilioni 25 kusaidia juhudi za afua katika utoshelevu wa chakula, miundombinu nyumbufu, ujasiriamali wa vijana na ubunaji nafasi za ajira na ufadhili wa kibunifu wa kukabiliana na tabianchi.

Bw. Adesina alitangaza kuwa AfDB ingetoa dola bilioni 12.5 na akatoa wito kwa washirika wa Afrika kusaidia na salio la dola 12.5 bilioni.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres aliunga mkono azma ya Afrika ya kukabiliana na hali hiyo, akisema kuwa kuwekeza katika kukabiliana na hali hiyo katika Afrika kungenufaisha ulimwengu mzima.

Bw. Guterres alikariri maoni yake ya ufunguzi ya COP27 (opening remarks) yaliyopokelewa vyema ambapo aliziomba serikali kutoza kodi ya faida ya ghafla ya makampuni za visukuku na kutumia fedha kuwasaidia "watu wanaokabiliana na kupanda kwa bei ya chakula na nishati na kwa mataifa yanayopata hasara na uharibifu unaotokana na mgogoro wa tabianchi.”

Mada: